Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) sekta
ya Kazi na Ajira na Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Vitendo Mahala
pa Kazi (Intership), uliofanyika hii leo Machi 5, 2020 katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wawakilishi wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa
Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya Kazi na Ajira na Uzinduzi
wa Programu ya Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi (Intership),
uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere
(JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama, akieleza jambo wakati wa Mkutano wa Mawaziri na
Wadau wa Utatu wa SADC sekta Kazi na Ajira uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax
akizungumza wakati wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta ya
Kazi na Ajira uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata
utepe alipokuwa akizindua rasmi Programu ya Mafunzo kwa vitendo Mahala
pa Kazi kwa wahitimu (Internship), iliyozinduliwia katika Mkutano wa
Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC Sekta ya Kazi na Ajira. Kushoto ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye
ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji
Wazee, Vijana Wanawake na Watoto kutoka Zanzibar, Maudline Castico.
Sehemu ya
Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) wakiimba wimbo wa SADC wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mkutano
wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya Kazi na Ajira na Uzinduzi wa
Programu ya Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi (Intership), uliofanyika
hii leo Machi 5, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwakabidhi Cheti kwa Bi. Agatha Masola ambaye ni mnufaika wa mafunzo
ya Vitendo Mahala pa Kazi.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji kanda
ya Kusini mwa Afrika (IOM) akielezea jambo kuhusu masuala ya Uhamiaji
kanda ya Kusini mwa Afrika.
Mmoja wa
Wanufaika wa Programu ya Mafunzo ya Uzoefu Mahala pa Kazi (Intership)
Bi. Mwamvita Kizima akieleza manufaa ya programu hiyo ilivyomsaidia
kupata uzoefu wa kazi. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji Wazee, Vijana Wanawake na Watoto kutoka Zanzibar, Maudline
Castico.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)
akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu pamoja na Maafisa
Waandamizi wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC Sekta ya
Kazi na Ajira.
**************************
Na: Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka
Mawaziri na Wadau wa Utatu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya Kazi na Ajira kuweka...
Mazingira wezeshi
yatakayowajengea vijana uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri.
Hayo yameelezwa
wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC wa
Sekta ya Kazi na Ajira pamoja na uzinduzi wa Programu ya Taifa ya
Mafunzo kwa Vitendo Mahala pa Kazi (Internship) iliyofanyika katika
Kitio cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar
es Salaam.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ikiwa ni “Kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mema Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu”.
Makamu wa Rais
alieleza kuwa ni muhimu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika wakawa na mikakati ya kuiwezesha nguvukazi ya Jumuiya hiyo na
hasa vijana kupata ujuzi stahiki utakaowawezesha kufanya kazi zenye
staha.
Alifafanua kuwa
taarifa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu mwenendo wa soko la
ajira kwa mwaka 2020, zaidi ya watu milioni 187.7 ikiwa sawa na asilimia
5.5 duniani hawana kazi na takribani wafanyakazi bilioni 2 ikiwa sawa
na 61.2% wanafanyakazi kwenye sekta isiyo rasmi na zaidi ya watu milioni
267 ikiwa ni sawa na asilimia 22 ambao kati yao wana umri wa miaka 15
hadi 24 na hawapo kwenye mafunzo wala ajira.
“Sisi kama
Jumuiya ya SADC tunalazimika kuwa na mikakati itakayowezesha nguvukazi
ambao kwa idadi kubwa ni vijana na wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia
60 katika jumuiya yetu, hivyo kama Jumuiya hatuna budi kuwekeza katika
kuwajengea uwezo vijana ili waweze kushiriki kikamilifu katika ukuzaji
wa uchumi wa nchi za ukanda huo,” alisema
Alisema kuwa
Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto ya ajira kwa
wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu nchini iliamua kuanzisha programu
ya taifa ya kukuza ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kuweza
kujiajiri na kuajiriwa.
“Niwasihi wenzetu
katika nchi za SADC ambao bado hawajaanzisha utaratibu huu, wajifunze
kutoka Tanzania na wakiona utaratibu huo unafaa wautelekeze kwa manufaa
ya vijana wa jumuiya hiyo,” alisema
Sambamba na hayo
Makamu wa Rais amewapongeza waajiri katika sekta binafsi na sekta ya
umma kwa kushirikiana na Serikali katika kuwajengea uwezo
vijana kujifunza maadili, mtazamo chanya kuhusu kazi pamoja na tamaduni
za kuishi mahali pa kazi na Kuwapatia uzoefu wa kazi unaohitajika na
waajiri.
Kwa upande wake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Programu ya
Taifa ya Kukuza Ujuzi nchini kwa vijana wa kitanzania imewasaidia vijana
wengi kujiandaa na kuingia katika soko la ajira ikiwemo sekta muhimu za
kipaumbele kama vile Ujenzi, Ukarimu, teknolojia ya habari, mawasiliano
na utalii.
Aliongeza kuwa
Programu ya Mafunzo kwa Vitendo Mahali pa Kazi kwa wahitimu
imewanufaisha vijana zaidi ya 5,967 ambapo vijana 3,967 wamehitimu
mafunzo na kati yao vijana 1,827 wamepata ajira moja kwa moja na vijana
2,000 bado wanaendelea na mafunzo hayo.
Naye, Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt.
Stergomena Tax alieleza kuwa Serikali ya Tanzania imeonesha nia thabiti
ya kutatua changamoto ya ajira kwa kuanzisha programu ya kukuza ujuzi
kwa vijana lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo vijana.
“Nichukue fursa
hii kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi inazozifanya katika
kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, kwa kuwapatia mafunzo
yatakayowajengea uzoefu katika soko la ajira,” alisema Katibu Mtendaji
wa SADC Dkt. Tax
Mkutano huo wa
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeshirikisha
pia Wadau wa Utatu wa Jumuiya hiyo ikiwemo Jukwaa la Vyama vya Waajiri
Kusini mwa Afrika (SPSF), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Kusini mwa
Afrika (SATUCC), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Kimataifa
linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji kanda ya Kusini mwa Afrika (IOM).
No comments :
Post a Comment