**************************
Na Emmanuel J. Shilatu
Serikali ya awamu ya 5
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli imefanya mambo makubwa kwenye kila sekta. Yafuatayo ni baadhi
tu ya mambo makubwa ya... kishindo zaidi yaliyofanyika ndani ya miaka 4 tu.
MAPATO
Tangu tupate Uhuru
mwaka 1961 hadi mwaka 2015 makusanyo ya mapato ya nchi kwa mwezi
hayajawahi kuzidi Tsh. Bilioni 700 ila ndani ya miaka 4 kuanzia 2015 –
2019 makusanyo ya mapato kwa mwezi mmoja yamefika Tsh. Trillion 1.9 .
Hii maana yake mianya ya upotevu imedhibitika, uwezo wa nchi kimapato
umeimarika na hivyo uwezo wa Serikali kuwahudumia Wananchi wake
utaongezeka pia.
AFYA
Kuanzia mwaka 1961
hadi 2019 sawa miaka 54 kulikuwa na hospitali za wilaya 70 ila ndani ya
miaka 4 kuanzia 2015 – 2019 jumla ya hospitali za wilaya 69 zimejengwa
na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli na vinatoa
huduma za afya.
Tangu mwaka 1961 –
2015 sawa na miaka 54 kulikuwa na vituo vya afya 150. Ndani ya miaka 4
kuanzia 2015 – 2019 jumla ya vituo vya afya 381 vimejengwa na vinafanya
kazi.
Hivyo ndani ya miaka 4
tu zimejengwa Zahanati 227, hospitali za wilaya 69 na vituo vya afya
381 sawa na jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 677.
UMEME
Mtandao wa umeme uliosambaa kwa umbali wa kilomita zaidi ya 69,204.39 na kufikisha upatikanaji wa umeme kuwa asilimia 67.5
Leo hii Taifa
linajenga umeme kwenye bwawa la umeme la Nyerere la Mto Rufiji ambao
utazalisha umeme megawatts zaidi ya 2115. Huu ni umeme mkubwa kuzidi
umeme uliopo tangu tupate Uhuru.
USAFIRISHAJI NA MIUNDO MBINU
Kwa zaidi ya miaka 30
nchi haikuwa na ndege zake ila ndani ya miaka 4 kuanzia 2015 – 2019
zaidi ya ndege mpya 8 zimenunuliwa na zinaendelea kutoa huduma ya
usafirishaji.
Tangu tupate Uhuru
Watanzania tunatumia treni ya Dizeli lakini ndani ya miaka 4 Serikali
imeanza ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha standard gauge (SGR)
kutoka Dar hadi Mwanza. Utakuwa usafiri wa haraka kwani unatumia umeme,
unaobeba mizigo mingi na nafuu zaidi.
Tangu Uhuru tumekuwa
tukitumia miundombinu ya Wakoloni lakini leo Taifa linajenga miundombinu
ya kisasa ya flyovers ya pale Tazara, Ubungo interchange, reli ya SGR
na madaraja yanayopita ama kukatiza katikati ya bahari na maziwa.
Leo hii nchi nzima
Kuna ujenzi wa viwanja vya ndege, ujenzi wa barabara na upanuzi wa
bandari za Dar es salaam, Mtwara, Tanga na kwenye maziwa makuu nchi
nzima.
ELIMU
Kwa zaidi ya miaka 30
Elimu yetu ilikuwa ya kulipia ila leo hii ndani ya miaka 4 tunashuhudia
Elimu bure ikitolewa kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Hakika
hiki ni zaidi ya kishindo cha awamu ya 5.
No comments :
Post a Comment