……………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema mtumishi wa umma asiyetaka kufuata maadili ya
utumishi pamoja na maelekezo ya viongozi wake hafai kufanyakazi katika
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Aliyasema hayo
jana jioni (Alhamisi, Machi 5, 2020) wakati alipozungumza na watumishi
wa Halmashauri ya Mji Korogwe na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa TTC Korogwe akiwa kwenye ziara ya kikazi
mkoani Tanga.
Waziri Mkuu
alisema uaminifu na uadilifu ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele
na watumishi wa umma nchini, hivyo aliwataka watumishi hao wasijiingize
kwenye mambo ambayo hayana tija katika utumishi wao.
Alisema
Serikali inataka kila mtumishi wa umma nchini awajibike kwa kufanya kazi
kwa bidii na kufuata maadili ya kiutumishi na kwamba haitomvumilia
mtumishi ambaye ni mwizi, mbadhilifu, mvivu na haitosita kumchukulia
hatua.
“Watumishi
mnatakiwa muwahudumie wananchi bila ya ubaguzi wa aliyenacho na
asiyekuwa nacho kwa sababu wananchi wote wana haki sawa ya kuhudumiwa,
hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.”
Pia, Waziri Mkuu
amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa ahakikishe
anawasimaia wakuu wa idara katika kupanga ratiba za kwenda vijijini
kuwasikiliza wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero
zinazowakabili.
Akizungumzia
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, Waziri Mkuu
alisema Serikali ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo hilo na
kuwataka wananchi waendelee kuwa na subra wakati suala hilo
linashughulikiwa.
Waziri Mkuu
alisemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya
kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote
nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.
Kuhusu suala la
upatikanaji wa umeme, Waziri Mkuu alisemamaeneo yote nchini yakiwemo ya
wilaya ya Korogwe yatasambaziwa umeme kupitia Mradi wa Nishati Vijijini
(REA).
Alisema wakati wa
usambazaji wa huduma hiyo wananchi hawatowajibika kulipia gharama za
nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari gharama
hizo zimeshabebwa na Serikali. “Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli
anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama ya
sh. 27,000 tu.”
Kwa upande wao,
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava na Mbunge wa Korogwe Mjini,
Mary Chatanda waliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, elimu
na pia waliiomba iwasaidie katika kutatua changamoto ya barabara, maji
na umeme.
Awali, Waziri
Mkuu aliweka jiwe la msingi kwenye mradi wa shamba la ufuta Mkomazi na
kujionea miundombinu ya umwagiliaji. Pia Waziri Mkuu alizindua miradi ya
ghala la kuhifadhia nafaka Mombo na alifungua maktaba ya chuo cha
Ualimu Korogwe.
No comments :
Post a Comment