Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,
akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Ssingi Kimanzichana Magharibi
iliyopo katika jimbo lake.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kilimahewa iliyopo katika
jimbo lake na kuwapatia zawadi ya madaftari.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdallah Ulega (Kulia) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
akipanda mti nje ya jengo la ofisi ya Serikali ya kijiji Kilimahewa
Muonekano wa jengo la ofisi ya
Serikali ya Kijiji cha Kilimahewa lililopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani
Pwani ambapo ujenzi wake hadi sasa umegharimu Shilingi Milioni 40
……………………………………………………………………………………..
Bodi ya Korosho
yatakiwa kulipa Shilingi Milioni 16 inazodaiwa na Kijiji
cha Kimanzichana
Kaskazini kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani
baada ya kukodi ghala la kijiji hicho kwa ajili ya kuhifadhi pembejeo za
kilimo za zao la korosho.
Akizungumza
mapema wiki hii wakati wa ziara ya kutembela maendeleo ya vijiji vya
Kimanzichana Kaskazini na Kilimahewa viliyopo katika wilaya hiyo, Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga ameutaka uongozi wa bodi hiyo kuhakikisha unailipa
Serikali ya kijiji cha Kimanzichana Kaskazini kiasi hicho cha fedha ili
kiweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Aidha katika
ziara hiyo Naibu Waziri Ulega amepata fursa ya kutembelea shule za
msingi Kimanzichana Magharibi, Kilimahewa na Shule ya Sekondari Mkamba
na kuzungumza na wanafunzi huku akiwataka kuweka bidii katika masomo
yao.
Mbali na
kuzungumza na wanafunzi hao Naibu Waziri Ulega ambaye ni Mbunge wa Jimbo
hilo la Mkuranga ametoa zawadi ya madaftari katika shule hizo ikiwa ni
sehemu ya ahadi aliyotoa ili kuongeza tija kwa wanafunzi hao waweze
kufanya vizuri zaidi katika masomo yao kwa kuwa na vifaa muhimu shuleni.
Halikadhalika
Mhe. Ulega ametembelea pia jengo la ofisi ya Serikali ya Kijiji cha
Kilimahewa ambapo ujenzi wake hadi sasa umegharimu Shilingi Milioni 40
na kutoa mchango wa Shilingi laki Tano kwa ajili ya kuendeleza ujenzi
huo na kupanda mti nje ya jengo la ofisi hiyo.
Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Mkuranga Mkoani Pwani yupo katika ziara ya kikazi jimboni humo kwa ajili
ya kukagua shughuli mbalimbali na miradi ya maendeleo.
No comments :
Post a Comment