Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamis Kigwangalla akiongea na watendaji pamoja na watumishi wa Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya hafla ya uvishwaji Menejimenti ya
Mamlaka hiyo.
Sehemu ya Wajumbe wa Menejimeti ya
NCAA waliovalishwa vyeo waakisikiliza hotuba wa Waziri wa Maliasili na
Utalii katika sherehe hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi
wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abihudi Kaswamila (aliyevaa
suti) akimvalisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi
anayesimamia utawala na Rasilimali watu Bw. Samson Ntunga.
Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt
Freddy Manongi akitoa taarifa kwa Waziri wa Maliasili na utalii Dkt
Hamis Kigwangalla ( hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa sheria ya
jeshi Usu katika utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
…………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu-NCAA
Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameshuhudia uvishwaji vyeo
kwa
menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikiwa ni
utekelezaji wa sheria kwa taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili
na Utalii kujiendesha kijeshi katika usimamizi wa Rasilimali za
wanyamapori.
Katika
sherehe hiyo wajumbe 15 wa menejimenti ya Ngorongoro walivishwa vyeo
ambapo idadi hiyo inajumuisha Naibu Makamishna wa uhifadhi wawili na
Makamishna wasaidizi Waandamizi wa uhifadhi 13.
Katika hafla
hiyo Waziri Kigwangalla ameielekeza menejimenti ya NCAA kutumia mafunzo
mbalimbali ya kijeshi waliyoyapata na kuhakikisha kuwa wanazingatia
nidhamu ya kazi, kasi katika utekelezaji wa majukumu na kuzingatia
mtiririko mzuri wa amri hasa kwa watumishi walioko chini yao ili
kuhakikisha kuwaa utendaji kazi inaimarishwa na kutatua changamoto
ndogondogo kwa uharaka na kijeshi usu.
Mhe.
Kigwangalla emesema kuwa sambamba na mafunzo mbalimbali ambayo viongozi
wa sekta za uhifadhi wamekuwa wakiyapata katika vyuo vya jeshi usu vya
Mlele na Mbulumbulu wizara yake itashirikiana na Jeshi la Polisi ili
kuwapa kozi ya uongozi wa masuala ya kijeshi katika chuo cha Polisi
Moshi ili kuongeza ufanishi wa usimamizi wa mifumo ya kijeshi katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Mwenyekiti wa
Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Profesa Abihudi Kaswamilla
amemhakikishia Waziri Kigwangalla kuwa, bodi anayoiongoza itaendelea
kusimamia utekelezaji wa mfumo wa jeshi usu kwa watendaji wa NCAA ili
kuhakikisha kuwa majukumu makuu ya uhifadhi, utalii na maendeleo ya
jamii yanatekelezwa ipasavyo.
Kamishna wa
Uhifadhi wa NCAA Dkt. Freddy Manongi amebainisha kuwa Mamlaka hiyo
itaendelea kusimamia uteekelezaji wa mfumo wa jeshi usu kwa watumishi wa
Mamlaka hiyo ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inayochangia fedha za
kigeni kwa asilimia 25 na pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 17
inazidi kuimarika na kuongezeka.
Viongozi
wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Gambo, wakuu wa Wilaya za Ngorongoro na Karatu, Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saimon Sirro, Kamishna wa Uhifadhi
wa TANAPA Dkt Allan Kijazi na viongozi wengine kutoka vyombo vya ulinzi
na Usalama.
No comments :
Post a Comment