Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo
Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolea na Benki ya CRDB wa
matrekta manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh.
Milioni 65 kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani
Tanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya
matrekta hayo Emmanuel Urio ambaye ni mkulima. Makabidhiano
hayo yalifanyika kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo
la Mwelya Sisal Estate la Korogwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo
Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa na Benki ya NMB wa
matrekta 11 na matrela yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni moja, kwa
Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani,
Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya matrekta
hayo Greyson Nyari , Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge Mkoa wa Tanga
kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate
la Korogwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua matrekta manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani
ya sh. Milioni 65 yaliyotolewa kwa mkopo na Benki ya CRDB kwa kwa Vyama
Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Mheshimiwa
Majaliwa aliyakabidhi matrekta hayo kwa wakulima kwenye shamba la mkonge
la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate la Korogwe Tanga,
Machi 5, 2020.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo
Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa kwa mkopo na Benki ya NMB wa
matrekta 11 na matrela yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni moja, kwa
Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani,
Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge mkoani Tanga, Greyson Nyari (wa pili
kulia) akionyesha ufunguo wa moja ya matrekta aliyokabidhiwa. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment