Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wanawake
wajasiriamali mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Wanawake
Wajasiriamali kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Katibu Mkuu Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea chimbuko la Siku ya
Wanawake Duniani katika ufunguzi wa maonesho ya wanawake wajasiriamali
mkoani Simiyi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony
Mtaka akieleza jitihada za mkoa katika kuhakikisha wanawake wanawezesha
wanawake kujikwamua kiuchumi wakati wa ufunguzi wa maonesho ya wanawake
wajasiriamali mkoani Simiyi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya
washiriki wa Msafara wa Kijinsia kutokomeza ukatili ilioanzia mkoani
Latavi na kupoita katika mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iirnga,
Tabora, Shinyanga na kumalizikia katika Wilaya za Maswa na Bariadi
mkoani SImiyu wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akiupokea Msafara
huo mkoani Simiyu.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Simiyu
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
kuwa
atazitaja Halmashauri ambazo hazitatoa mikopo kwa wanawake kwa aslimia
50 ya mapato yake kuwa adui wa maendeleo ya wanawake.
Waziri Ummy
ameyasema hayo mkoani Simiyu wakati akifungua maonesho ya wanawake
wajasiriamali na kupokea msafara wa kijinsia wa Twende Pamoja
uliomalizikia mkoani humo.
Waziri Ummy
amesema kuwa suala la kutenga fedha kwa ajili ya mikopo ya wanawake,
Vijana na watu wenye ulemavu sio suala la hiari bali lazima kwani lipo
kisheria.
“Kabla ya
tarehe 30 June tutazitaja Halmashauri zote ambazo hazikutoa mikopo kwa
wanawake kwa asilimia 50 na tutazitaja kama maadui wa maendeleo ya
wanawake” alisema
Ameongeza kuwa
wanawake wakiwezesha watachangi kwa silimia kubwa ukuaji wa uchumi kwani
kwa takwimu zilizopo asilimia 60 ya chakula kinazaliswa na wanawake na
Serikali inaendelea kuhakikisha wanawake wanawezehswa kiuchumi.
“Tutahakikisha
wanawake wanawezeshwa kiuchumi kwani tumepitisha Sheria ya utoaji mikopo
bila riba kwa wanawake ili kuwawezesha kupata mikopo itakayowasaidia
kuinua biashara zao” alisema
Aidha Waziri
Ummy mawataka wamamchi kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyotolea
katika maneno yao na hasa wananume kujitokeza kutoa taarifa kwani
vitendo hivi hawafanyiwi wanawake pekee bali hata wanaume wanafanyiwa
vitendo vya kikatili.
“Niwatake
wanawake kutokuwa sababu ya kufanyiwa vitendo vya kikatili kwani kuna
wanawake wamekuwa akiona vitendo vya kikatili kuwa suala la kawaida ”
alisema
“Natoa mfano
kuna utafiti umefanyika na kubaini katika wanawake waliulizwa swali kuwa
kama ikitokea ukauunguza mboga je ukipigwa na mumeo kwa kitendo hiko ni
wanawake asilimia 20 walijibu ni sawa lakini sio sawa kabisa” alisema
Akizumgumza
kuhusu chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Katibu Mkuu
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amaeema wananwake walikuwa
ahawapati nafasi stahiki katika jamii ukilinganisgawa na wanaume hivyo
Umoja wa Miatfa uliona ni jambo sahihi kuwa na Siku maalum ya
kukumbushana kuhusua masuala ya wanawake.
No comments :
Post a Comment