Friday, March 6, 2020

MAJALIWA AZINDUA MAKTABA MPYA CHUO CHA UALIMU KOROGWE



Muonekano wa moja ya Eneo la kujisomea katika Maktaba mpya ya Chuo cha Ualimu Korogwe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa Tehama wa Chuo cha Ualimu Korogwe baada ya kuzindua Makataba ya Chuo hicho
Chumba cha kompyuta katika Maktaba mpya ya Chuo cha Ualimu Korogwe
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Maktaba mpya ya Chuo cha Ualimu Korogwe, Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigela, Mbunge wa Korogwe Mjini Mhe. Mary Chatanda na Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo
…………………………………………………………………………………………………………
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Machi 5, 2020 amezindua maktaba mpya ya Chuo cha Ualimu Korogwe kilichopo Mkoani Tanga.
Akizungumza na baadhi ya walimu tarajali na wanafunzi aliowakuta katika maktaba hiyo
mara baada ya kuizindua Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao kuitumia vyema maktaba hiyo kwa lengo la kujipatia maarifa na kuongeza uwezo katika taaluma.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimkaribisha Waziri Mkuu amesema
Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 338 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maktaba hiyo ambayo ujenzi wake ukianza kwa Micjango ya Wananchi wa Korogwe.
Katibu Mkuu huyo amesema Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuunga mkono juhudi za wananchi ambao walichanga shilingi milioni 1.9 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.
“Wananchi wa Korogwe waliona umuhimu wa chuo hiki kuwa na maktaba na wakaanza kuchanga fedha na kuanza ujenzi” amesema Dkt. Akwilapo.
Mmoja wa walimu tarajali katika Chuo cha Ualimu Korogwe Emanuela Bombo ameishukuru Serikali kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa maktaba hiyo kwani itasaidia katika ujifunzaji.
Maktaba hiyo ina vifaa vya kisasa pamoja zikiwemo kompyuta ambazo zinawezesha matumizi maktaba mtandao na kwamba Maktana itatumiwa na walimu tarajali zaidi ya 1000 ambao wanasoma masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA na pia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wa wilaya ya Korogwe.

No comments :

Post a Comment