Mkurugenzi wa Kurugenzi Utafiti
na sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Suleiman Misango
akizungumzia kuhusu ripoti iliyotolewa na IMF jijini Arusha mara baada
ya kufunga semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha iliyokuwa
ikifanyika kwa siku tano jijini humo.
……………………………………………
IMF Imetoa mhutasari wa taarifa
yao kuhusu mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania na matarajio yake
ile taarifa yao fupi imeelezea mwenendo wa
uchumi kwa mwaka 2019
wakieleza kuwa utakuwa kwa asilimia 6 na wakaongeza kuwa umekuwa
ukifanya vizuri.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya Utafiti na sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk.
Suleiman Misango wakati akizungumza jijini Arusha mara baada ya kufunga
semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha iliyokuwa ikifanyika
kwa siku tano jijini humo.
“Sisi tunasema kwa hapo baadaye
uchumi wetu utakuwa zaidi, Takwimu zetu za hivi karibuni Robo ya kwanza
mwaka 2019 inaishia machi, ya pili inaishia Juni na ya tatu inaishia
septemba kwa wastani katika kipindi hicho uchumi wetu ulikuwa kwa
asilimia 6.9 na tunatarajia kwamba ile robo ya nne ambayo ndiyo inafunga
mwaka tunaamini ukuaji wa uchumi wetu utakuwa kwa asilimia 7.
Dk. Suleiman Misango amesema kwa
siku za Baadaye tunakubaliana na IMF kwamba kama tutakwenda na utaratibu
na nguvu kama hizi ukuaji wa uchumi wetu utakuwa zaidi asilimia 7 kwa
siku za karibuni na siku za muda wa kati .
Amesema kutokana na uwekezaji
mkubwa unaofanywa na serikali katika sekta za Nishati , Miundombinu,
Afya, Elimu, Mawasiliano , Umeme na Shughuli zingine za uzalishaji mali
uwekezaji huu ndiyo wezeshi kwa ajili ya Shughuli mbalimbali za
kiuchumi,ndiyo maana hali ya ukuaji wa uchumi imekuwa ikienda vizuri.
“Ili kuweza kuharakisha maendeleo
unahitaji nishati ya umeme, Ili kuharakisha maendeleo unahitaji
kuboresha miundombinu ya Reli na Barabara ili kuharakisha maendeleo
unahitaji kuboresha Elimu, Afya na mambo mengine”Amesema Dk. Misango.
Amesema ripoti hiyo pia
imezungumzia mfumuko wa bei ambapo IMF wamekiri kabisa na kuridhika
kwamba mfumuko wa bei umekuwa mdogo na mwaka jana wastani ulikuwa 3.5,
Mwezi wa Januari kulikuwa na ukuaji wa asilimia 3.7 tunatarajia mfumuko
wa bei utaendelea kuwa mdogo na IMF wenyewe wamesema kabisa kuwa mfumuko
wa bei utaendelea kuwa mdogo chini ya malengo yetu ya muda wa kati ya
asilimia 5.
Ameeleza kuwa ripoti hiyo pia
imezungumzaia pia Sekta ya nje ya Tanzania katika biashara na nchi
zingine ambapo wameridhika na mwenendo wa sekta yetu katika mauzo ya
nje. Yameendelea kuwa mazuri na vilevile akiba ya fedha za kigeni
imeendelea kuwa ya kutosha, tunaweza kuagiza bidaa na huduma kutoka nje
kwa miezi mitano ambapo sisi pia takwimu zetu za hivi karibuni
zinaonesha tunaweza kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi sita.
No comments :
Post a Comment