IGP Sirro akiwa na mfadhili huyo Fouad Martis na Mkuu wa mkoa wa Arusha wakitembelea majengo hayo ya makazi ya Askari wa jeshi la Polisi ambayo yanatarajiwa kukamilika mwezi wa nne mwaka huu. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Jeshi
la polisi nchini limewaonya viongozi wa madhehebu ya dini kutoingilia
mambo ya kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
kwani halitasita kumchukulia hatua kali yeyote Yule atakayekiuka agizo
hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro aliyasema hayo juzi alipokuwa
akiweka jiwe la msingi katika jingo la nyumba za Askari polisi
zinazoendelea kujengwa katika eneo la kikosi cha kutuliza ghasia FFU
kata ya Muriet jijini Arusha.
Alisema
kuwa kila kiongozi wa imani ya madhehebu yoyote ya kidini antakiwa
kufanya shughuli zake katika eneo lake la kazi na kwamba jeshi hilo
limejipanga kikamilifu kukabiliana na yeyote Yule atakayesababisha
kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani na utalivu hapa nchini.
“Wewe
kama askofu,Mchungaji Padri au Sheikh shughuli zako za kiimani zifanye
kanisani au msikitini na hata wewe mwananchi fanya shughuli zako bila
kutenda au jaribio la kiuhalifu sisi hatutojali endapo utaenda kinyume
na taratibu zilizopo tutakufikia na kukukamata popote ulipo kwani hakuna
aliye juu ya sheria”alisisitiza
Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi aliwataka askari polis nchini kuhakikisha
wanafanyakazi zao kwa weledi uaminifu na watende haki kwani kumekuwa na
changamoto kubwa ya kutokutenda haki kwa baadhi ya askari hao hivyo
wazingatia kiapo chao kwenye utendaji wao wa majukumu ya kila siku.
Akatoa
wito kwa wananchi wote nchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu
watende na kufanya shughuli halali ambapo amekemea tabia ya wazazi na
walezi ambao wamekuwa wakiwatetea watoto wao wanajihusisha na matukio ya
kiuhalifu hivyo amewataka kuwalea kwenye maadili mema.
Awali
akimkaribisha IGP mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alilipongeza
jeshi hilo mkoani hapa chini ya usimamizi wa kamanda wa polisi mkoani
hapa Jonathan Shana kwa usimamizi mzuri na kupambana na uhalifu mkoani
hapa.
Kadhalika
Gambo alimuomba mkuu wa jeshi la polisi kukipandisha hadhi kituo cha
polisi Muriet ambapo hapo hapo Sirro alikubali ombi hilo na kukipa hadhi
kituo hicho kuwa kituo cha polisi cha kiwilaya Muriet na ataleta OCD na
OCS katika kituo hicho ili wananchi wapate huduma za kipolisi kwa kuwa
kuna wananchi wengi na huduma nyingi wanapata kituo kikuu cha polisi
jijini Arusha.
Akaahidi
kuhakikisha kuwa wanaendeleza kuuweka mkoa huo kuendelea kuwa salama na
Amani ambapo pia akawataka wananchi mkoani hapa kutoa ushirikiano kwa
jeshi hilo kwenye mapam,bano ya kiuhalifu kwa kutoa taarifa za
kiuhalifu.
“IGP
Sirro naliomba jeshi la polisi mjenge mazingira mazuri kwa askari
kuwajengea makazi na kuboresha maslahi yao kwani kwa kufanya hivyo
askari watakuwa na morali ya kufanyakazi hivyo uhalifu hautakuwa na
nafasi mkoani hapa na nchini kwa ujumla wake”alisema
Kwa
Upande wake Balozi wa Heshima wa serikali ya Dubai Fouad Martis ambao
ndio wafadhili wa mradi huo wa nyumba za polisi wenye thamani ya dola za
kimarekani laki mbili alisema kuwa wao kama wawekezaji hapa nchini
wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni kurudisha kwa jamii faida kidogo
wanayoipata.
Nae
Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya CRJE ya China Tumainiel Seria
alisema kuwa jengo hilo lina nyumba sita ikiwemo sebule,vyumba viwili
vya kulala na jiko na kwamba ujenzi umefikia asilimia 50 na wanaahidi
kuukamilisha mwezi wa nne mwaka huu.
No comments :
Post a Comment