Thursday, March 5, 2020

ERIKALI YA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA UFARANSA KATIKA MAZINGIRA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akisalimiana na Maseneta kutoka Ufaransa waliomtembelea Ofisini kwake Luthuli katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiskiliza kwa makini wakati alipokutana na Maseneta kutoka Ufaransa waliotembelea Ofisini kwake Luthuli jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kiongozi wa Maseneta hao Senator Hervé Maurey.
Sehemu ya Maseneta kutoka Ufaransa waliomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu Ofisni kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Maseneta hao wako Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiwa katika picha ya pamoja na Maseneta kutoka Ufaransa waliomtembeleaOfisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Alichoshika mkononi ni medali aliyopewa na Maseneta hao.
………………………………………
Serikali ya Tanzania imeahidi kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala yote yanayohusu mazingira  na Serikali ya Ufaransa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Mussa Zungu wakati
alipokutana na Maseneta kutoka Ufaransa waliomtembelea katika Ofisi yake ndogo iliyopo Luthuli jijini Dar es Salaam.
“Tanzania inapenda kushirikiana na Ufaransa kwenye masuala ya mazingira wala msiwe na hofu wala kigugumizi kuanzia leo tutataandaa maeneo ya vipaumbele ya kushirikiana nyinyi na sisi na tuweze kufanya kazi kwa pamoja” alisitiza Waziri Zungu.
Akijibu swali la Seneta mmojawapo aliyeuliza kuhusu suala la ukataji miti kwa Tanzania, Waziri Zungu alisema kuwa anawahakikishia Maseneta hao kuwa kwa sasa hakuna tena kuharibu mazingira ikiwepo suala la ukataji miti kwa sababu Wizara inasimamia suala la mazingira ipasavyo. 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira  (NEMC) akiongea katika Mkutano huo amesisitiza kuhusu uwekezaji wa nishati mbadala ili kuweza kumkomboa Mwananchi wa kawaida kabisa aliyepo kijijini pia akasema kuhusu suala la kupatiwa teknolojia ya urejelezaji taka.  
Maseneta hao wameshukuru kwa ukarimu waliopatiwa wakati wa ziara yao Nchini Tanzania na kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ukarimu huo na kuahidi kushirkiana nao kwa dhati kabisa katika kutatua changamoto mbalimbali za mazingira kwa pamoja. Maseneta hao sita kutoka Nchini Ufaransa wako Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.

No comments :

Post a Comment