Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Julieth Kidemi akiwaelimisha wakazi wa
Mbuyuni kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni kuhusu madhara mbalimbali
yatokanayo na biashara za magendo wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha
wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi.
Kampeni hii imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11
Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga,
Mtwara na Lindi.
Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akiwaelimisha wakazi wa
kata ya Kimbiji wilayani Kigamboni kuhusu madhara mbalimbali yatokanayo
na biashara za magendo wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi
kuhusu athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Kampeni hii
imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020
katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na
Lindi. na Lindi.
Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Ernest Mngube akiwaelimisha wakazi wa kata ya Kimbiji
wilayani Kigamboni kuhusu madhara mbalimbali yatokanayo na biashara za
magendo wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za
magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Kampeni hii imeanza kufanyika
tarehe 3 na itamalizika tarehe 11 Februari, 2020 katika maeneo
mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
*******************************
Na Veronica Kazimoto
Kigamboni
Wakazi
na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi
katika kata za Somangila, Kimbiji na Pemba Mnazi zilizopo Wilaya ya
Kigamboni jijini Dar es Salaam wameelimishwa kuhusu athari za magendo
yanayopitishwa kinyume na sheria katika maeneo hayo.
Elimu
hiyo imetolewa wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu
athari za magendo katika ukanda wa Bahari ya Hindi iliyoandaliwa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inafanyika maeneo mbalimbali
katika mikoa ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga, Mtwara na Lindi.
Akizungumza
na wakazi hao katika maeneo ya Buyuni na Kimbiji wilayani Kigamboni,
Afisa Kodi Mkuu Rose Mahendeka kutoka mamlaka hiyo, amewaambia wakazi
hao kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapoona bidhaa za magendo ikiwa
ni pamoja na kuepuka kutumia bidhaa hizo kwani zinaweza kuwa na madhara
kwa afya zao.
“Ndugu
zangu athari za magendo siyo tu kukwepa kodi ya serikali, lakini pia
bidhaa hizo zinazopita katika njia zisizo rasmi, zinakuwa
hazijathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya
Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) na hivyo zinaweza kuwaletea madhara kiafya,”
alisema Mahendeka.
Naye,
Afisa Forodha kutoka TRA Ernest Mngube, amewaasa wafanyabiashara
wanaojishughulisha na biashara za magendo kuacha tabia hiyo mara moja
kwani wakibainika licha ya kuchukuliwa hatua za kisheria, watataifishiwa
bidhaa zao ikiwa ni pamoja na vifaa vilivyotumika kubeba au kuhifadhi
bidhaa hizo.
“Ni
muhimu wafanyabiashara mtambue kwamba kupitisha bidhaa katika njia
zisizo rasmi ni kinyume na sheria na mkibainika siyo tu mtachuliwa hatua
kwa mujibu wa sheria bali bidhaa zenu zitataifishwa pamoja na vifaa
kama gari, pikipiki, mashua zinazotumika bidhaa hizo na hata majengo
yatakayokutwa yamehifadhi magendo hayo,” aliwaasa Mngube.
Mgumbe
amezitaja namba ambazo wananchi wanaweza kutoa taarifa kila wanapoona
biashara za magengo katika maeneo yao ambazo ni 0746 23 24 91, 0800 75
00 75, 0800 78 00 78 au kutuma ujumbe wa whatsapp kwenda namba 0744 23
33 33 au kutuma barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz.
Kampeni
maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu athari za magendo katika ukanda wa
Bahari ya Hindi imeanza kufanyika tarehe 3 na itamalizika tarehe 11
Februari, 2020 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Saalam, Pwani, Tanga,
Mtwara na Lindi ikiwa na lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara na
wananchi kwa ujumla madhara mbalimbali yatokanayo magendo hayo.
No comments :
Post a Comment