……………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
HALMASHAURI Ya
Chalinze,Mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto katika shughuli za ugani
ikiwemo usafiri wa uhakika kuwafikia wakulima ambao wapo vijijini na
vitongoji.
Aidha kuna vijiji 31
ambavyo havina maofisa hivyo kutokana na changamoto hizo wakulima
wamekuwa hawapati huduma yenye tija kwa kushindwa kufikiwa na maafisa
ugani mara kwa mara.
Changamoto hizo
zimewekwa bayana na mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze,Amina Kiwanuka
katika makabidhiano ya pikipiki kumi zenye thamani ya mil.25 kwa
maofisa ugani wa vijijini na magari ya halmashauri mapya mawili yenye
thamani ya zaidi ya milioni 290.
Alieleza,kutokana na
changamoto hiyo kupitia idara ya kilimo halmashauri ya Chalinze
imejiwekea malengo hadi kufikia 2021/2022 iweze kununua pikipiki 50
kutoka kwenye bajeti za mapato ya ndani kwa ajili ya maofisa ugani wa
vijiji na kata.
“Pikipiki hizi
zitawasaidia maofisa ugani hawa kuwatembelea wakulima kwa wakati na
kuwapa huduma ambazo zitawawezesha kuongeza tija katika sekta ya
kilimo”alifafanua Amina.
Hata hivyo Amina
alielezea, maofisa hao wataweza kutumia pikipiki hizo kwenda kuhudumia
katika vijiji ambavyo havina maofisa ugani.
Nae mwenyekiti wa
halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu alieleza, halmashauri hiyo
ilianza kutenga bajeti ya pikipiki mwaka wa fedha 2018/2019 na kununua
pikipiki 15 zenye thamani ya milioni 37.5 na kupewa maofisa ugani wa
kata.
“2019/2020 zimenunuliwa pikipiki hizi kumi za milioni .25 na kupewa maofisa ugani wa vijiji vya pembezoni !:’
Na pia tumetenga milioni 32.4 kwa ajili ya pikipiki 12 kwa mwaka 2020/2021″‘:
Zikatimu alisema
,kutokana na umuhimu wa usafiri ili kurahisisha utendaji kazi magari
yaliyonunuliwa nayo yanakwenda kusaidia kusukuma kazi za idara
mbalimbali ambazo zinahitaji matokeo kupitia usafiri.
Kwa upande wake ofisa
ugani wa kijiji cha Kimange, Aloyse Jumanne aliiahukuru halmashauri kwa
kuiona changamoto ya ukosefu wa usafiri na kuifanyia kazi.
Alibainisha,usafiri
huo unakwenda kujibu kero za wakulima ambao walikuwa hawafikiwi kwa
wakati na kujikuta wakishindwa kunufaika na kilimo cha kisasa
No comments :
Post a Comment