Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa
Azzan Zungu akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge
wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo.
Azzan Zungu akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge
wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa
Sima akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge wakati wa kipindi cha
maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo.
Sima akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge wakati wa kipindi cha
maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa
Azzan Zungu na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Mussa Sima wakifuatilia kipindi
cha maswali na majibu wakati wa kikao cha Bunge leo.
Azzan Zungu na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Mussa Sima wakifuatilia kipindi
cha maswali na majibu wakati wa kikao cha Bunge leo.
****************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Serikali inatarajia kuweka mikakati ya kupanda miti zaidi
ya milioni moja kwenye eneo la Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu iliyopo nchini.
Pia amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti na kuitumia kama fursa ya ufugaji nyuki akitahadharisha kuwa mamilioni ya hekta za misitu yamepotea
katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2010 kutokana na ukataji miti ovyo.
katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2010 kutokana na ukataji miti ovyo.
Zungu ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Welezo Mhe. Saada Mkuya Salumu aliyetaka kujua mkakati gani wa Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Mheshimiwa mwenyekiti nchi zilizoendelea zinaemit carbon na athari kubwa zinatokea kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hivyo zinaharibu mazingira lakini zimekuwa zinasita kufinance kwenye climate change, Serikali yetu imejipangje kukabiliana na matatizo haya?,” aliuliza.
Akifafanua zaidi, Waziri Zungu alisema kuwa ni kweli baadhi ya nchi kubwa duniani zimejitoa kwenye mkataba wa tabianchi kutokana na maslahi yao binafsi
na kuwa nchi zilizobakia zikiongozwa na Ufaransa na Qatar zimeanzisha Mfuko wa dola milioni 100 zitakazotolewa kwa nchi zitazohitaji kuboresha mazingira yao.
na kuwa nchi zilizobakia zikiongozwa na Ufaransa na Qatar zimeanzisha Mfuko wa dola milioni 100 zitakazotolewa kwa nchi zitazohitaji kuboresha mazingira yao.
Alisema kuwa Tanzania imeshaanza mkakati wa kuziomba fedha hizo sambamba na kuandaa program mbalimbali za kuhakikisha nchi yetu inafaidika nazo na kulinda mazingira.
Aidha waziri huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa inaandaa mkakati wa kupanda miti katika kila wilaya zote za
hapa nchini ili kuboresha mazingira.
hapa nchini ili kuboresha mazingira.
“Kwa sasa tumeandaa mkakati wa kupanda miti kwa kila wilaya na si tu kupanda lakini na kuitunza ili isije ikafa kwani inapandwa kwa gharama kubwa na inakufa,
halmashauri nyingi zinahamasika kupanda miti lakini baada ya muda mfupi inakufa. Tutaweka aina maalumu za miti kwa kila wilaya ambayo itafaa,” alifafanua.
halmashauri nyingi zinahamasika kupanda miti lakini baada ya muda mfupi inakufa. Tutaweka aina maalumu za miti kwa kila wilaya ambayo itafaa,” alifafanua.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janet Mbene aliyeulitaka kujua ni lini Serikali itaanza kutoza ada kwa mkaa unaosafirishwa nchi za nje ili iweze kurejesha mazingira katika hali yake Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Mussa Sima alisema kwa sasa Serikali haisafirishi mkaa unaotokana na miti kwenda nje ya nchi na gharama za kurejesha maeneo yaliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo mkaa, zitatokana na mapato yanayopatikana kupitia tozo mbalimbali
zilizoainishwa kwenye Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 ikiwepo asilimia 5 ya ushuru wa Halmashauri inayotozwa kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu.
zilizoainishwa kwenye Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 ikiwepo asilimia 5 ya ushuru wa Halmashauri inayotozwa kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu.
Aidha, tozo nyingine zitatokana na tozo za ukaguzi wa biashara ya mkaa unaotokana na mabaki ya miti au mimea (briquettes) ambao unaruhusiwa kwenda nje ya nchi.
“Ni kweli uchomaji wa mkaa utokanao na miti kwa kiasi kikubwa unatumia miti ya asili pamoja na mapori ya akiba na ni dhahiri, ukataji wa miti hauendi sambamba
na upandaji wa miti na hii ina athari kubwa sana kwenye mazingira yetu ikiwemo kuendelea kupotea kwa bioanuai, kupungua kwa mvua na kukauka kwa vyanzo
vya maji,” alisema.
na upandaji wa miti na hii ina athari kubwa sana kwenye mazingira yetu ikiwemo kuendelea kupotea kwa bioanuai, kupungua kwa mvua na kukauka kwa vyanzo
vya maji,” alisema.
Naibu Waziri aliongeza kuwa biashara hiyo inafanyika kwa mujibu wa Sheria yamMisitu ya Mwaka 2002, Kanuni za mwaka 2004 na Miongozo mbalimbali.
Aidha, usafirishaji wa mkaa nje ya nchi umezuiliwa kwa mujibu wa kifungu namba 16 cha Sheria inayozuia Usafirishaji wa baadhi ya bidhaa nje ya nchi (The Exports
Control Act, {CAP 381 R. E 200} pamoja na makatazo mengine.
Control Act, {CAP 381 R. E 200} pamoja na makatazo mengine.
Aliongeza kuwa Tangazo la Serikali Na. 417 la tarehe 24/05/2019 kifungu Na. 21 (1) limetoa zuio kwa mtu yeyote kusafirisha mkaa kwenda nje ya nchi isipokuwa
mkaa mbadala (charcoal briquettes) na kwa kibali maalumu kutoka kwa Waziri mwenye dhamana.
mkaa mbadala (charcoal briquettes) na kwa kibali maalumu kutoka kwa Waziri mwenye dhamana.
No comments :
Post a Comment