Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na
Nyumba Stela Tulo akimfafanulia jambo Naibu Msajili Mahakama Kuu Charles
Magesa alipotembelea Banda la Msajili wa Mabaraza wakati wa Maonesho ya
Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma
leo 04 Feb 2020.
Msajili Msaidizi wa Baraza la
Ardhi na Nyumba Kanda ya Kati Shilly Repenti (Kulia) na Afisa Ardhi
Anord Mkude wakitoa elimu kwa wateja waliotembelea Banda la Ofisi ya
Msajili wa Mabaraza Winfrida Mtengule (Kushoto) na Asha Komba wakati wa
Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere
Square Dodoma leo 04 Feb 20202.
Afisa Ardhi wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anold Mkude akimsikiliza
kwa makini Wakili Upendo Mwakatika wakati wa Maonesho ya Wiki ya Sheria
yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma leo tarehe
4 Feb 20202 (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
********************************
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Msajili wa
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo amewataka wananchi kutumia
vyombo vilivyo wekwa kwa mujibu wa sheria katika kutafuta haki kwenye
migogoro ya ardhi.
Tulo alisema hayo
leo tarehe 4 Februari 2020 katika maonesho ya Wiki ya Sheria
yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Alisema, kumekuwa
na tabia ya baadhi ya wananchi walio kwenye migogoro ya ardhi kwenda
kwa viongozi kama vile Wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi wengine
kutafuta haki kwenye migogoro ya ardhi na kuacha vyombo vilivyowekwa kwa
mujibu wa sheria jambo alilolieleza linachangia migogoro ya ardhi
kutapata suluhu kwa wakati.
Kwa mujibu wa
Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini, vyombo vinavyohusika
kisheria kutoa haki katika migogoro ya ardhi ni kuanzia ngazi ya Baraza
la Ardhi la Kijiji, Kata, Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya,
Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi na Mahakama ya Rufaa.
Alisema, iwapo
wananchi walio kwenye migogoro ya ardhi watafuata utaratibu wa kutumia
vyombo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria wataweza kupata haki zao na
wakati huo na kuepuka kupoteza muda mwingi wa kukata rufani kuhusiana na
migogoro ya ardhi.
Aidha, Tulo
alitumia fursa ya Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kuwataka
wananchi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye
maonesho hayo ili kupata elimu kuhusiana na Mabaraza ya Ardhi na hivyo
kujua taratibu za kutafuta wakati wa migogoro ya ardhi.
Naye Afisa Ardhi
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Arnold Mkude alisema
Ofisi ya Msajili wa Mabaraza ya Ardhi nchini inayatumia maonesho ya Wiki
ya Sheria kama njia ya kutoa elimu kwa wananchi wote wanaotembelea
Banda la ofisi hiyo ili kufahamu kazi na namna Mabaraza ya Ardhi
yanavyofanya kazi.
Hata hivyo,
alisema tangu kuanza Maonesho hayo wananchi wengi wa,mekuwa wakijitokeza
kwenye banda hilo kwa nia ya kutaka kupata ufahamu kuhusiana na
Mabaraza ya Ardhi na kubainisha kuwa wengi wao wameonesha kutokuwa na
uelewa wa Mabaraza ya Ardhi au taratibu za kufuata wakati wa kushuhulika
na migogoro ya ardhi.
No comments :
Post a Comment