Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. George
Masaju akibadilishana mawazo na Mawakili wa Serikali , Tunu Temu na
Anna Mkongwa, Wakati Mhe. Masaju alipotembelea banda la Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Viwanja vya Nyerere Square Jiji
Dododma, ambako
wiki ya utoaji elimu kuhusu masuala ya kisheria .
Pamoja na mambo mengine Mhe. Masaju alipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
kufungua Ofisi katika Mikao Nane na akashauri Ofisi hizi zienee
Mikoa yote kutoka na mahitaji makubwa ya huduma za Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu.
………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu,Nyerere Square, Dodoma
Wadau mbalimbali wakiwamo, Majaji,
Wanasheria na Wananchi wa kawaida, wameiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali kufanya kila liwezakanalo kuhakikisha kwamba, kunachapishwa
toleo jipya la mapitio ya sheria mbalimbali.
Kwa mujibu wa wadau hao, tolea la
mwisho lilichapishwa mwaka 2002 na hakujawa na chapisho jipya, jambo
linalowapatia ugumu mkubwa wa rejea wakati wa utoaji wa maamuzi
mbalimbali.
Maoni na mapendekezo ya wadau hao,
ni kuitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba,
jitihada zinafanyika za kuwa na toleo jipya ili pamoja na mambo mengine
kuondoa hatari ya kutoa uamuzi au ushauri kwa kutumia sheria ambayo
tayari imekwisha kufanyiwa marekebisho au imefutwa kabisa.
Zaidi ya wadau kumi ambao
wamefika katika Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilipo
katika Viwanja vya Nyerere Square, wameelezea shida na mkanganyiko
wanaoupata wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na muda wanaopoteza
kufanya marejeo ya sheria ambazo zimeshafanyiwa maboresho lakini hazipo
katika mpangilio unaoeleweka.
Wakati huo huo Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepongezwa kwa kufungua Ofisi zake katika
Mikoa kadhaa ili kurahisha upatikanaji wa huduma za kisheria.
Pongezi hizo zimetolewa na
Mhe.Jaji George Masaju wakati alipofika katika banda la Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali lilipo katika viwanja ya Nyerere Square.
“Niwapongeze kwa hatua hii nzuri
ya kuanza kufungua Ofisi mikoani kwa sababu ni muhimu sana kwa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawa katika kila Mkoa na ikiwezekana kila
katika Halmashauri za Wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma”
Akasema Mhe. Jaji Masaju.
Akasema kuwa, kufisha Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hadi ngazi ya wilaya inawezekana ingawa
ni kazi nzito kutokana na uhaba wa Bajeti lakini linawezekana ikiwa
Halmashauri zitashirikishwa ili ziingize katika mipango yao ya Bajeti
kwa sababu wanahitaji huduma ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ipo katika Mikoa ya Arusha, Tanga, Tabora, Mtwara, Kagera,
Kilimanjaro,Mwanza, na Mbeya
No comments :
Post a Comment