Mkurugenzi Mtendaji kutoka TECDEN (Tanzania
Early Childhood Development Network) Bw. Bruno Ghumpi akifafanua jambo
wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango Kutokomeza ukatili
dhidi ya wanawake na watoto kilichofanyika Februari 6, 2020 katika
Ukumbi wa mikutano wa Flomi hotel Morogoro.
Mratibu wa MTAKUWWA kutoka Wizara ya Elimu, Bi. Sylvia Chinguwile akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Mratibu wa Taifa
wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na
Watoto (MTAKUWWA) Bi. Happiness Mugyabuso (katikati) pamoja na Katibu wa
kikao hicho Bw. Mwendesha Makelemo na Mratibu wa Mpango huo kutoka
TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga (wa kwanza kushoto) wakifuatilia hoja za
kikao hicho.
Afisa Maendeleo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akiwasilisha mada kuhusu
mila na desturi zinazowagandamiza watoto na wanawake wakati kikao hicho.
Wajumbe wa kikao
cha kujadili utekelezaji wa Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya
Wanawake na Watoto wakifuatilia hoja wakati wa kikao hicho.
Afisa Maendeleo
ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto Bi. Rennie Gondwe akiwasilisha mada wakati wa kikao
hicho.
Mratibu wa Mpango
wa Kutokomea Kukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kutoka
TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga akifafanua hoja wakati wa kikao kazi cha
kujadili utekelezaji wa Mpango huo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments :
Post a Comment