Thursday, February 6, 2020

MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA LEO



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza mwanamasumbwi, Salim Mtango wa Tanga ambaye Januari 31, 2020 alifanikiwa kumshinda kwa TKO bondia wa Thailand, Suriya Tarakhun na kunyakuwa mkanda wa dunia wa UBO. Bondia huyo alitembelea bunge jijini Dodoma Februari 6, 2020 kwa mwaliko wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (mwenye koti la bluu kulia). Wa tatu kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu wake, Juliana Shonza. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo Mijini, Angelina Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, bungeni jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba , bungeni jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu, bungeni jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments :

Post a Comment