Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Ofisini kwake jijini
Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga,akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dodoma
wakati akitoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari Ofisini kwake jijini
Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga,amesema kuwa wametangaza kuanza usajili wa wadau wote katika mnyororo mzima wa uongezaji thamani ya mazao ya kilimo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa
habari amesema kuwa Lengo la usajili huo ni
kutaka kuwa na takwimu sahihi ya wadau mbalimbali wanaotoa huduma
katika sekta ya kilimo nchini.
Ametaja wadau hao
kuwa ni pamoaj na wakulima, watoa huduma mbalimbali za pembejeo,
wasindikaji, wafanyabiashara za mazao, Taasisi za fedha, watoa huduma wa
sekta binafsi katika kilimo kama Asasi za kiraia na mashirika ya ndani
na nje ya nchi yanayotoa huduma kwenye kilimo, wenye viwanda vya
kuongeza thamani, watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa zana za
kilimo n.k.
Amesema kuwa Usajili huo utafanyika kwa njia ya kidigitali kwenye mtandao wa www.kilimo.go.tz na kupitia simu za kiganjani.
Waziri Hasunga amesema kuwa Usajili huo utaanza rasmi tarehe 15 Februari, 2020 na kukamilika tarehe 14 Aprili, 2020.
Kupitia usajili
huo, takwimu na taarifa muhimu zitapatikana kwa ajili ya kuendeleza
kilimo zikiwemo watoa huduma za pembejeo, huduma za ugani, taasisi za
fedha, wasindikaji na wenye viwanda, watengenezaji, wauzaji, wasambazaji
wa zana za kilimo, na hivyo, kuweza kujua kiwango cha uwekezaji katika
sekta ya kilimo.
Mhe Hasunga
amesema kuwa Wizara ya kilimo inaendelea na usajili wa wakulima kote
nchini ili kuweza kuwatambua na kurahisisha utoaji wa huduma za ugani,
mitaji kwa ajili ya kilimo, upatikanaji wa pembejeo na kupata taarifa
sahihi za uzalishaji.
Amesema kuwa
Usajili wa wakulima Awamu ya Kwanza hadi kufikia Januari, 2020 umefikia
jumla ya wakulima 1,279,884 na usajili unaendelea.
Kati yao,
wakulima wa mashamba makubwa ni 147 wakewemo 101 wa zao la kahawa, chai
12, Mkonge 22 na miwa 12; na wakulima wadogo ni 1,279,737 wakiwemo
309,000 wa zao la Korosho (98.4%), 305,260 wa Kahawa (95.4), Pareto
10,687 (112%), Mkonge 6,885 (91%), miwa wakulima 6,745 (96.4), chai
wakulima 31,092%, Tumbaku wakulima 53,757 (107.5%) na Pamba wakulima
556,306 (92.7).
Usajili wa
wakulima Awamu ya Pili utaanza kwa kutumia mfumo wa kidigitari kwa
kusajili taaarifa muhimu za wakulima ikiwemo ukubwa wa mashamba yao,
aina ya teknolojia wanazotumia katika uzalishaji, wadau wanatoa huduma
za kifedha, huduma za ugani, pembejeo, n.k
Waziri Hasunga
amesema kuwa Maendeleo ya Kilimo hasa katika kuongeza uzalishaji na tija
kwa wakulima yanategemea kwa kiasi kikubwa matumizi sahihi ya mbegu
bora, mbolea na viuatilifu.
Licha ya umuhimu huo, bado kuna changamoto ya upatikanaji na matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikilinganishwa na mahitaji.
Aidha,
inakadiriwa kuwa wakulima nchini wanapoteza takribani asilimia 30 ya
mazao kabla na baada ya mavuno kutokana na magonjwa na milipuko ya
visumbufu mbalimbali vya mimea.
No comments :
Post a Comment