Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na mameneja
(hawapo pichani) wakati wa kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi
wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Kulia ni meneja wa
TEMESA mkoa wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri na kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko Mhandisi Adelard Kweka.
Baadhi ya mameneja wa mikoa na
vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA waliohudhuria kikao cha
mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha
2019/2020 wakisikiliza kwa umakini taarifa mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Meneja wa Uchumi kutoka Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Frederick Gwanchele akisoma taarifa kwa
mameneja wa vituo na mikoa wa Wakala huo wakati wa kikao cha mapitio ya
taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Arusha.
Mameneja wa mikoa na vituo wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa katika picha ya pamoja na
Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Maselle (katikati) mara
baada ya kumaliza kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu
mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
PICHA ZOTE NA TEMESA (ARUSHA)
No comments :
Post a Comment