Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akipokea zawadi ya
ua kutoka kwa mtumishi wa wizara hiyo Bi.Tukupsya Mwamasage alipowasili
katika ofisi za wizara Mji wa Serikali Jijini Dodoma, mara baada ya
kuapishwa jana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe
Magufuli.
Katibu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto) akisitiza
kwa viongozi wa menejimenti (hawapo pichani)kuwa amedhamiria kufanya
mageuzi ya kiutendaji alipofanya kikao na viongozi hao,baada ya kuwasili
katika ofisi ya wizara iliyopo Mji wa Serikali Mtumba,Jijini Dodoma
baada ya kuapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe
Magufuli,kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo Dkt.Ally Possi.
Katibu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto)
akisalimiana kwa furaha na wafanyakazi wa wizara alipowasili katika
ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma,mara
baada ya kuapishwa kwake jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John
Pombe Magufuli.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akitoa taarifa
fupi kuhusu Idara za Kisekta na Vitengo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo
Dkt.Hassan Abbasi wakati wa kikao cha utambulisho wake kwa viongozi wa
menejimenti leo Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa jana na Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi (kushoto) akipokea
nyaraka mbalimbali zinahusu ofisi ya Katibu Mkuu kutoka kwa Naibu Katibu
Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Ally Possi ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya
ofisi mara baada ya kikao na viongozi wa menejimenti aliporipoti leo
Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM.Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi amewataka viongozi
wa menejimenti wa Wizara hiyo kufanya mageuzi kwa kuwa sekta za
wizara
hiyo zimebeba ushawishi mkubwa kwa nchi na dunia.
Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo
Jijini Dodoma baada kuwasili katika ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba na kufanya mazungumzo na viongozi wa Menejimenti kwa
lengo la kupata taarifa fupi ya kisekta na makabidhiano ya ofisi.
“Wizara hii imebeba sekta muhimu sana katika nchi ambazo ni soft power na smart power
mfano sekta ya Sanaa na Michezo ni burudani na sekta hizi zikisimamiwa
vizuri taifa hili litazidi kuwa la amani na furaha pamoja na uchumi
utaongezeka,tutaandaa matamasha ya kitaifa ya burudani kama JAMAFEST
ambayo yatashirikisha wasanii na wachezaji sisi ni watumishi wa umma
lazima tuoneshe wananchi utendaji wetu na ningependa tuache kufanya kazi
kwa mazoea,”alisema Dkt.Abbasi.
Akiendelea kuzungumza katika
kikao hicho, Dkt. Abbasi alisema kuwa anatarajia kuona utendaji wa
pamoja (team work) na utendaji wa kujituma pasipo kuchoka,pia
alisisitiza anategemea kutumia vipaji na ubunifu.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi alipokuwa akifanya
makabidhiano alimweleza Dkt. Abbasi changamoto mbalimbali za wizara
ikiwemo ya uhaba wa fedha katika uendeshaji wa Uwanja wa Taifa na pamoja
na Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kuwa na changamoto
katika uendeshaji, umuhimu wa programu hiyo sababu kuwa ni ya kimataifa
na faida zake utakaposimamiwa vyema na kukamilika.
“Nakupongeza kwa mapinduzi makubwa
unayoyafanya katika Idara ya Habari hakika kazi ni nzuri haswa katika
kuisemea Serikali ningeomba kwa upande wa usimamizi wa taaluma ya habari
na Vitengo vya Mawasiliano Serikalini huko nako nguvu inahitajika ili
kuwa na utendaji wenye usawa katika uwajibikaji wenye tija,’’alisema
Dkt.Possi.
Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu, Bw.Marceline Patrick alimpongeza Katibu Mkuu huyo na
kumweleza kuwa watumishi wote wamefurahia uteuzi wake na wana imani nae
katika kusimamia mabadiliko ya sekta za wizara na wapo tayari kumpa
ushirikiano ili kufanikisha hilo.
Halikadhalika mmoja wa
wafanyakazi wa wizara hiyo kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Bibi
Hadija Kisubi alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kumteua Dkt.Abbasi kuwa Katibu
Mkuu katika wizara hiyo sababu ni mchapakazi na anaamini kuwa atafanya
mabadiliko makubwa katika wizara katika maeneo yote yenye changamoto.
No comments :
Post a Comment