Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu
walipokutana kwa ajili ya mazungumzo Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando ya
Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh
Gebeyehu. Mazungumzo hayo yamefanyika Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando
ya Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.
kushoto aliyevaa kilemba ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi
Azizi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu (Katikati) akiwa na ujumbe wake katika
mazungumzo baina yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb).Mazungumzo hayo
yamefanyika Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando ya Mkutano wa 33 wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.
********************************
Tanzania
imeishauri Nchi ya Ethiopia kuchukua hatua ya kuchunguza kiini cha raia
wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu na kwa
njia zisizo halali
jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa ambao wanakamatwa katika
nchi wanazopita kama wahamiaji haramu ikiwemo Tanzania.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John
Kabudi ametoa ushauri huo Addis Ababa Ethiopia anakohudhuria mkutano wa
33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na kukutana na Waziri
wa Mambo ya Nje wa Ethiopia kando ya mkutano huo Dkt. Workneh Gebeyehu
na ili kuchukua hatua za kudhibiti idadi ya raia wake wanaondoka nchini
humo na kukamatwa katika mataifa mengine Tanzania ikiwemo.
Prof. Kabudi
amesema Mpaka sasa takribani raia zaidi ya 1,300 wanashikiliwa katika
magereza mbalimbali nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea kukamatwa
ikiongezeka jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa katika
magereza ya nchi hiyo.
Ameongeza
kuwa katika mazungumzo hayo Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua
hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa wafungwa na wahamiaji haramu
wan chi hiyo wanaoshikliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika baada
ya majadiliano ya kina na kitaalamu.
Akizungumza
kupitia kwa msemaji Waziri wa mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh
Gebeyehu amekiri kuwepo kwa tatizo la vijana wan chi yake kuondoka
nchini humo kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito
wakielekea katika nchi za kusini mwa Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa
serikali ya nchi hiyo itachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali
hiyo.
Pia
ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano wake katika suala la wahamiaji
haramu kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu raia wa Ethiopia
wanaoshikiliwa Tanzania na kwamba wana imani kuwa mazungumzo
yatakayofanyika yatasaidia kuwarejesha raia hao nchini Ethiopia kwa njia
ya pamoja watakayokubaliana.
Kando na
masuala hayo ya wahamiaji haramu pia Prof. Kabudi na Dkt. Workneh
wamezungumzia masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na
Ethiopia ikiwa ni pmaoja na mashirikiano katika masuala ya
anga,miundombinu na ubadilishanaji wa utaalamu kuhusu ujenzi wa mabwawa
ya umeme ili kuziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo katika
nyanja ya Uchumi.
No comments :
Post a Comment