Leo tasnia ya habari nchini
hususani redio, inaungana na wanahabari wengine duniani katika
Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Redio Duniani ambayo huadhimishwa kila
mwaka ifikapo
Februari 13.
Natumia fursa hii kuwapongeza
wadau wote wa redio nchini kwa kuendelea kutumia chombo hicho
kuwajulisha Watanzania matukio mbalimbali yanayotokea hapa nchini na
duniani kwa ujumla.
Aidha, nawahakikishia wadau kuwa
Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa
na redio hapa nchini ikiwemo kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa
ajili ya uanzishaji wa redio nyingi zaidi.
Hadi Februari 12, 2020 jumla ya
redio 204 zimesajiliwa hapa nchini ambapo redio 183 ni zile zinazorusha
matangazo katika masafa ya redio na 21 ni redio za mtandao hali
inayowafanya Watanzania kupata haki yao ya msingi ya Kikatiba.
Nawatakia wadau wote maadhimisho
mema na sherehe za mwaka huu iwe chachu zaidi ya kuboresha vipindi na
habari zinazotolewa na redio zetu.
No comments :
Post a Comment