…………………………………………………………………………………………………………
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Jumatatu tarehe 17 Februari
2020 atakwenda katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya
kurudisha umiliki wa ekari 750 kwa manispaa hiyo kama ilivyoelekezwa na
Rais Magufuli.
Rais John Pombe
Magufuli alitoa siku saba kuanzia jumanne iliyopita kwa Wizara ya Ardhi
kurejesha miliki ya eneo hilo kwa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni
kufuatia kufuta miliki ya eneo hilo ili kuwa chini ya Serikali.
Uamuzi wa Lukuvi
ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli alilolitoa jumanne wiki hii baada ya kuzindua jengo la
Manispaa ya Kigamboni na lile la Mkuu wa Wilaya hiyo yaliyoko eneo la
Gezaulole jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa
njia ya Mtandao leo tarehe 13 Februari 2020 akiwa Abu Dhabi, Falme za
Kiarabu anakohudhuria Kikao cha Mawaziri wa Afrika Kuhusu Masuala ya
Nyumba na Maendeleo ya Miji Lukuvi alisema, jumatatu atakuwa ofisi za
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya
kutekeleza agizo la Rais kuhusiana na urejeshaji miliki ya ardhi kwa
halmashauri hiyo.
‘’Jumatatu tarehe
17 Februari 2020 saa tano asubuhi nitakuwa ofisi za Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kutekeleza agizo la mhe Rais la
kukabidhi ardhi ambayo iko katika eneo la Kigamboni’’ alisema Lukuvi
Kwa mujibu wa
Rais Magufuli, pamoja na kufuta umiliki wa eneo hilo ili kuwa chini ya
Serikali lakini umiliki wake haujarerejeshwa katika Manispaa ya
Kigamboni na kutaka miliki hiyo kurejeshwa ndani ya wiki moja ili
wananchi wapange wanavyotaka.
Hata hivyo,
Magufuli alitahadharisha ardhi hiyo isije ikatumika vibaya kwani si ya
viongozi bali ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kigamboni.
No comments :
Post a Comment