Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha
Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali Cherestino Msolla
(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Nsajigwa
Mwankenja walipofanya ziara ya mafunzo katika Jeshi la Magereza jana
Februari 12, 2020.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha
Ulinzi wa Taifa wakitembelea sehemu mbalimbali katika Kiwanda cha Gereza
Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha
Ulinzi wa Taifa wakizungumza na mfungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani
wa fani ya ushonaji katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Ukonga
kama inavyoonekana katika picha.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha
Ulinzi wa Taifa wakitoka katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga
kuendelea na ziara yao ya mfunzo katika maeneo mbalimbali ya Jeshi la
Magereza.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza,
SSP. Amina Kavirondo akiwasilisha andiko linalohusu majukumu ya Jeshi
hilo mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo
pichani).
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha
Ulinzi wa Taifa wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali nkuhusu
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza ikiwemo program za
urekebishaji, jana Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Askari wa Kikosi
Maalum cha Magereza kikionesha onesho la ukakamavu mbele ya Maafisa
Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(NDC) walipotembelea Makao
Makuu ya Kikosi hicho jana, jijini Dar es Salaam.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha
Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiburudika na matunda ya madafu katika
ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.
Kamishna wa Magereza, Uwesu
Ngarama(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa
Washiriki waliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
jana(waliosimama mstari wa nyuma) kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Tanzania(wa pili toka kushoto walioketi) ni Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo
cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali Cherestino Msolla
(kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Katungu(Picha zote na
Jeshi la Magereza).
No comments :
Post a Comment