Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),akiangalia moja ya darasa
linalotumika kufundishia wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania
wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza
ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na
Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akikagua dawati katika moja ya darasa
linalotumika kufundishia wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania
wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza
ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na
Jeshi la Polisi,wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Salum Hamduni(kulia) baada ya kukagua moja
ya chumba vinavyotumika kutoa huduma ya malazi kwa wanafunzi katika
Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya hapo chuoni
lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze kufaidika na huduma
zinazotolewa na Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi
baada ya kuwasili katika Shule ya Polisi Tanzania wakati wa ziara yake
aliyoifanya hapo chuoni lengo kusisitiza ufundishaji makini ili jamii
iweze kufaidika na huduma zinazotolewa na Jeshi la Polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameutaka uongozi wa
Shule
ya Polisi Tanzania kuwafundisha ueledi wapelelezi ili kuweza kupunguza
msongamano wa mahabusu na kesi ambazo zinasababishwa na upelelezi usio
na kiwango.
Masauni ameyasema
hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya kutembelea Shule ya Polisi
Tanzania lengo ikiwa kusisitiza ufundishaji makini ili jamii iweze
kufaidika na huduma za Jeshi la Polisi.
“Mheshimiwa Rais
Dkt. John Magufuli alipokua akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya
Sheria aligusia suala la wapelelezi kuwa chanzo cha mlundikano wa
mahabusu katika magereza yetu na mimi hii leo nimetoka gereza la Arusha
nimeongea na wafungwa na mahabusu nao wanalalamikia upelelezi wa kesi
zao kupindishwa na mbaya zaidi wengine wamehukumiwa vifungo kwa ajili ya
upelelezi usio makini.Ni tatizo kubwa haiwezekani Rais huyu alalamike
kila siku sasa maagizo ya serikali kwa chuo hiki jitahidini kupika
vizuri wapelelezi wenu vizuri,tumpumzishe Rais wetu ana mambo
mengi,timizeni tu wajibu wenu”amesema Masauni
Akizungumza
katika ziara hiyo Kaimu Kamandanti Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar
amesema wamechukua maelekezo ya serikali na wanaahidi kuyafanyia kazi
ili yaweze kuleta tija huku akitaja idadi ya wanafunzi waliopo shuleni
hapo wakisomea fani mbalimbali.
“Shule yetu kwa
sasa ina wanafunzi 856 kati yao wanaume 725 na wanawake ni 131 ambao
wako katika mafunzo mbalimbali na wote wanaendelea vizuri na masomo”
amesema Kamishna Msaidizi Omar
Katika ziara hiyo
Naibu Waziri Masauni alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
shule hiyo ikiwemo sehemu za kulala,madarasa,uwanja wa paredi,vyumba vya
komputa na ukarabati bwalo la chakula.
No comments :
Post a Comment