Naibu waziri wa Afya akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Arusha leo(Happy Lazaro)
…………………………………………………………………………………………………
Happy Lazaro,Arusha
Serikali imezitaka
Taasisi na vyuo vya maendeleo ya jamii kuandaa programu za mafunzo ya
uanagenzi ambazo zitawezesha kutoa ujuzi na stadi muhimu zinazohitajika
katika viwanda .
Hayo yameelezwa na
Naibu Waziri Wizara ya afya ,maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto
dkt Faustine Ndungulile wakati akifungua mkutano Wa majadiliano ya
wadau kuhusiana utekelezaji Wa dhana ya uagenzi,yaliofanyika katika
ukumbi Wa mikutano Wa kimataifa (AICC)Jana ndani ya jiji LA Arusha
ambapo alisema kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kuliwezesha Taifa kuwa
na wahitimu mahiri na wenye ujuzi utakaochangia katika kufanikisha Azma
ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi Wa kati Wa viwanda
ifikapo 2025.
Alisema kuwa ,vijana
wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini wanaishia kuwa na Elimu ya kile
walichosomea badala ya ujuzi ambapo ndio unatakiwa kwa vijana wetu.
Alisema kuwa,ni
lazima sasa tuhakikishe kuwa tunawaandaa vijana wetu kuwa na ujuzi wa
kutosha kwani swala hill limekuwa ni changamoto kubwa kwa vijana walio
wengi na mwisho wake kuishia kubaki mtaani baada ya kuhitimu vyuo
mbalimbali.
Aidha Dokta Ndugulile
alisema kuwa,uwepo Wa uanagenzi ni suluhisho la kuhakikisha mifumo ya
Elimu inazalisha wataalamu mahiri wenye ujuzi au stadi zinazohitajika
katika solo la ajira kwenye uchumi wa viwanda.
“kila mmoja anatambua
kuwa serikali imeona umuhimu wa kushughulikia changamoto ya kuzalisha
wahitimu wasioajirika kwenye sekta rasmi na isiyorasmi kwa kuanzisha
dhana ya uanagenzi kwenye taasisi na vyuo vya maendeleo ya jamii ,hivyo
nawaomba sana wote kwa pamoja mhakikishe mnakuwa na ushirikiano wa
kutosha katika kufanikisha swala hili.” alisema Naibu Waziri.
Aliongeza
kuwa,utekelezaji wa dhana ya uanagenzi unategemea sana ushirikiano mzuri
uliopo kati ya taasisi au vyuo vya mafunzo na waajiri ambapo wote kwa
ujumla hutoa nadharia katika fani mbalimbali na kupitia viwanda,taasisi
za umma na za binafsi na mashirika wanachuo hupata fursa na kufanya kwa
vitendo wanayojifunza na kupata ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira .
Aidha alizitaka
taasisi hizo kuwaunganisha wanafunzi na wahitimu wa mafunzo ya
uanagenzi na taasisi zakifedha ili wapate mitaji na
vifaavitakavyowezesha kujiajiri
Akitoa mada ya juhudi
za serikali z ya kuboresha ujuzi wa wahitimu wa taaluma ya maendeleo ya
jamii na maendeleo ya jamii -ufundi Mkurugenzi msaidizi wa vyuo vya
maendeleo ya jamii Neema Ndoboka alisema vijana wengi wanaohitimu
vyuoni hawanaujuzi wa vitendo vya kile walichosomea hivyo kupelekea
vijana hao kukosa ajira .
“Unakuta kijana
anaelimu ya natharia (darasani ) ya hali ya juu lakini ukija kwenye
vitendo Hanna kitu hivyo ndio maana tumeamua kuanzisha swala hill LA
vijana wetu kufanya Kazi kwa kujitolea pindi wanapomaliza masomo yao
,pindi wanapojitolea inawasaidia kupata uelewa mzuri zaidi wa vitendo”
alibainisha Neema
Kwa upande wake Mkuu
wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru ,dkt.Bakari George alisema
katika kuelekea katika swala hill ni muhimu vijana waliopo mashuleni
kwanza waanze kujiandaa kifikra na awe na utayari wa kujifunza shuleni
pamoja na sehemu ya Kazi ambapo anaenda kujifunza kwa vitendo zaidi na
kupata ujuzi zaidi.
Aliongeza kuwa,kuna
haja kubwa ya taasisi na mashirika mbalimbali kuhakikisha wanakuwa na
ushirikiano wa kutosha kati yao na vyuo ili kuweza kutoa elimu kulingana
na mahitaji ya soko ili wanapohitimu waweze kuingia kwenye ajira moja
kwa moja .
No comments :
Post a Comment