Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro akimuelekeza jambo Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr.
Tigest Ketsela katikati wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo
katika maadhimisho ya Siku ya Madaktari Tanzania yaliyofanyika jana
kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro akiwa na Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam walipotembelea banda la Mkapa Foundation katika maadhimisho hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro kulia na Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela wakifurahia jambo, Kushoto ni Rebeca Stanley
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation Ellen Mkondya Senkoro wa
pili kutoka kushoto akiwa na Rahel Sheiza Mkurugenzi wa Miradi pamoja
na baadhi ma maofisa wa taasisi hiyo kutoka kulia ni Christina Godfrey
Afisa Sera na Uraghbishi Mkapa Foundation , Rebeca Stanley Afisa
Uhusiano na Mawasiliano Mkapa Foundation na kushoto
Rahel Sheiza
Mkurugenzi wa Miradi Mkapa Foundation katikati akiwa na Rebeca Stanley
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mkapa Foundation kushoto na Christina
Godfrey Afisa Sera na Uraghbishi Mkapa Foundation.
……………………………………………..
RAIS Dkt. John Magufuli
ameameipongeza taasisi ya Mkapa Foundation kwa kujenga nyumba za
madaktari 482 nchini kote ikiwa na jitihada za taasisi hiyo kutatua
changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchi Tanzania
Akizungumza Alhamisi (Februari
20, 2020) Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya
siku ya Madaktari
Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam , Rais Magufuli alisema naipongeza taasisi ya Mkapa Foundation
kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidiana na serikali kutatua matatizo
mbalimbali yanayoikabili sekta ya afya nchini.
“Serikali ya Awamu ya Tano
itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma
bora za afya nchini ili kuimarisha ustawi wa maisha ya wananchi na
Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kushirikiana vizuri na taasisi
zinazofanya kazi ya kusaidiana na serikali kutatua matatizo mbalimbali
katika sekta ya afya”.Amesema Rais DK. John Pombe Magufuli.
Taasisi ya Mkapa Foundation
katika mkakati wake wa kupunguza changamoto za sekta ya afya pamoja na
kujenga nyumba hizo katika vituo 268 nchini kote pia imejenga vyumba 11
vya upasuaji katika vituo 12 vya kutolea huduma ambapo ujenzi huo
umeambatana na kuweka vifaa, kuajiri watumishi na kutoa mafunzo stadi
kwa watumishi.
Mkapa Foundation imetoa ajira
2033 za wataalamu wa afya Kada mbalimbali 11 waliopangiwa kazi katika
mamlaka za Serikali za Mitaa 51 katika mikoa 22 na vyuo vya Afya 46
ambapo mpaka sasa watumishi 1397 wameshahusishwa katika utumishi wa
umma.
No comments :
Post a Comment