Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dk. Zainab Chaula akizungumza
na Julieth Mselle Afisa Huduma kwa wateja kutoka MSD wakati
alipotembelea katika banda la taasisi hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya
Madaktari Tanzania ukumbi wa Julius Nyerere Posta. jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dk. Zainab Chaula akimsikiliza
Julieth Mselle Afisa Huduma kwa wateja kutoka MSD wakati alipotembelea
katika banda la taasisi hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Madaktari
Tanzania ukumbi wa Julius Nyerere Posta. jijini Dar es salaam.
Julieth Mselle Afisa Huduma kwa wateja kutoka MSD akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu
wakati alipotembelea katika banda la taasisi yake katika Maadhimisho ya
Siku ya Madaktari Tanzania ukumbi wa Julius Nyerere Posta. jijini Dar
es salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu
akizungumza na baadhi ya wageni wakati walipotembelea katika banda la
taasisi yake katika Maadhimisho ya Siku ya Madaktari Tanzania ukumbi wa
Julius Nyerere Posta. jijini Dar es salaam.
Julieth Mselle Afisa Huduma kwa wateja kutoka MSD na Benjamin Massangya afisa Mawasiliano Mwandamizi MSD wakiwa katika banda lao.
………………………………………..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dk. Zainab Chaula ameiasa
Bohari ya Dawa nchini MSD kutotoa dawa bure kwa Hospitali , Vituo vya
Afya na Zahanati kote nchini badala yake walipe fedha kama utaratibu
unavyotaka na fedha zitakazopatikana kutokana na malipo ya dawa hizo
zifanye kazi ya kununua dawa zingine kwa ajii ya kuhudumia watanzania.
Dk. Chaula ameyasema hayo kando
ya mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Madaktari Tanzania uliofanyika
kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam jana wakati
alipotembelea banda la MSD ambao walishiriki katika maonesho ya taasisi
mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya afya.
Dk. Chaula amesema MSD ni wadau
muhimu katika afya za watanzania kwani ndiyo wenye wajibu wa kuhakikisha
dawa zinapatikana kote nchini na kila wakati kwenye hospitali zetu,
Vituo vya Afya na Zahanati hivyo ni muhimu wahakikishe fedha
zinazopatikana baada ya kusambaza dawa zifanye kazi ya kununulia dawa
zingine kwa mahitaji mengine ya baadae.
Ameipongeza MSD kwa kazi kubwa
inayofanya nchini na kuwataka kuendelea kuchapa kazi hiyo kwa weledi,
ari na umakini mkubwa kwa sababu kazi ikifanyika vizuri na malengo ya
afya bora kwa watanzania yatafikiwa vizuri nchini kote.
No comments :
Post a Comment