Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akikagua baadhi ya magari ambayo yamekamatwa na
Mamlaka ya Mapato Tunduma kutokana na kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na
magendo.
Baadhi ya magari ambayo yamekamatwa na Mamlaka ya Mapato Tunduma kutokana na kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magendo.
Kibarua wa mfanyabiashara wa
pembejeo Tunduma Issa Sanga akijaribu kuvusha Mbolea ya Ruzuku nchi
jirani ya Zambia kwa baiskeli ambapo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela ameagiza kufungwa kwa duka la mfanyabiashara huyo na
uchunguzi ufanyike.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akikagua risiti katika duka la Mfanyabiashara ambaye
alikutwa akifanya udanganyifu katika kutoa risiti
………………………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameagiza Afisa wa Jeshi la Polisi
wa Tunduma aliyekamatwa na gari alilomiliki kwa njia za magendo,
achukuliwe hatua za
kisheria haraka.
Brig. Jen.
Mwangela ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua magari na bidhaa
zilizokamatwa na Mamlaka ya Mapato katika Mpaka wa Tunduma ambapo pia
ameonyeshwa gari la Afisa wa Jeshi la Polisi wa Tunduma lililo kamatwa
kwa kulimiliki kwa njia za magendo huku taarifa zikionyesha
linasafirishwa kuelekea Nchi jirani ya Kongo.
“Afisa huyo wa
Polisi amesema kuwa gari hilo lilikuwa likitumika na Jeshi la Polisi kwa
kazi maalum lakini nimezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa amesema gari
hilo haliko katika utaratibu wa kipolisi wala halikuwa likifanya kazi za
serikali hivyo naagiza achukuliwe hatua za kisheria haraka sana.”,
amesema Brig. Jen. Mwangela.
Amesema kwa
kumiliki gari hilo kinyume na sheria na taratibu za Nchi kisha
kudanganya uhalali wa umiliki wake Afisa huyo wa Polisi anavunja sheria
za Nchi, anakwepa kodi, ana hujumu uchumi wa taifa na pia amelitia aibu
Jeshi la Polisi.
Brig. Jen.
Mwangela ameongeza kwa kuitaka Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe
kuhakikisha wana wakamata wote wanaokiuka sheria za Nchi hata kama ni
watumishi wa serikali huku akiviagiza vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa
wa Songwe kuongeza ulinzi katika eneo la Mpaka ili kuzuia Magendo.
Pia amewakumbusha
wananchi na wafanyabiashara wanaovusha bidhaa nchi Jirani wafuate
taratibu za Forodha, wananchi nao watoe taarifa za wale wanao kiuka
sheria kwakuwa watakao kamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Naye Kaimu Meneja
Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Songwe Anangisye Mtafya amesema wamekuwa
wakikamata magari ya magendo na mengine ambayo Watanzania wasio
waaminifu wamekuwa wakiyabadilisha na kuweka namba zisizo halisi.
Mtafya ameongeza
kuwa baada ya kusafishwa Mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma
kazi ya kukamata watorosha magendo imerahisishwa tofauti na zamani
ambapo nyumba zilikuwa zimejaa eneo la mpaka.
Wakati huo huo
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefanya ukaguzi wa
kushtukiza katika maduka ya biashara jirani na Mpaka wa Tanzania na
Zambia eneo la Tunduma na kukuta baadhi ya wafanyabiashara wakiuza
mbolea ya Ruzuku nchi jirani ya Zambia huku wengine wakitoa risiti zenye
udanganyifu.
Brig. Jen.
Mwangela ameagiza kufungwa kwa duka la pembejeo ambalo alimkuta
mfanyabiashara Issa Sanga akijaribu kuvusha mbolea ya Ruzuku Nchi jirani
ya Zambia na uchunguzi ufanyike ni mbolea kiasi gani amevusha hadi
sasa.
No comments :
Post a Comment