NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MAOFISA
waandikishaji,waandikishaji wasaidizi pamoja na maofisa uchaguzi wa
halmashauri na TEHAMA mkoa wa Pwani wameaswa ,kufuata miiko na sheria
zilizo chini ya Tume wakati wa utekelezaji wa zoezi la uboreshaji
daftari la kudumu la wapiga kura ,linalotarajiwa kuanza februari 14 na
kukamilika februari 20 mwaka huu.
Pamoja na hayo,
mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya
kuandikisha wapiga kura ,Jambo ambalo litaleta uwazi ila hawatakiwi
kuwaingilia watendaji hao wanapotekeleza wajibu wao .
Akifungua semina ya
mafunzo ya uandikishaji mkoani Pwani, ambayo ni ya siku moja ,kamishna
wa Tume ya Taifa ya uchaguzi ,Jaji mstaafu Longway Mary Harriet Chibibi,
alisema endapo atatokea ofisa atakaekiuka sheria zilizopo atachukuliwa
hatua kulingana na matakwa ya sheria iliyopo.
Alitoa wito, kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Tume hiyo ili waweze kufanya kazi zao ipasavyo wakati wa zoezi hilo.
Alisema ,mafunzo haya
ya jinsi ya kutumia mfumo wa uandikishaji yanalenga kuwawezesha maofisa
waandikishaji na maofisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo,TEHAMA
kupata uelewa wa jinsi ya kutumia kwa ufasaha BVR kit kwa ajili ya
uboreshaji wa daftari “:
“Na wao waweze kutoa
mafunzo hayo kwa maofisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata ambao nao
watatoa mafunzo hayo kwa BVR kit -operators na waandishi wasaidizi
ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura
vituoni.”:alifafanua Longway.
Nae mratibu wa
uandikishaji mkoani Pwani, Gerald Mbosoli aliwahakikishia wananchi kuwa
mkoa umejipanga kufikia maeneo yote lengwa hadi maeneo yasiofikika
kirahisi ikiwemo kisiwa cha Mafia na Delta huko Rufiji.
Mshiriki wa mafunzo
hayo ambae pia ni ofisa mwandikishaji wa halmashauri ya Mji wa Kibaha
,Jennifer Omolo alieleza, halmashauri hiyo ina mitaa 73,na vituo 122
hivyo watahakikisha vituo vyote vinapata waandikishaji
No comments :
Post a Comment