Katibu Mkuu Dkt.Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha afya mazingira (hawapo chuoni).
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha
afya mazingira kagemu wakimsikiliza katibu mkuu ambapo anewaahidi
kurudisha huduma ya chakula na kufanya ukarabati jiko la chuoni hapo
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenyr picha ya pamoja na wanachuo wa mwaka wa tatu wa chuo cha afya ya mazingira kagemu.
***************************
Na. Catherine Sungura-Kagera
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ameahidi
kurudisha chakula kwa wanachuo wote ili
kuondoa kupoteza muda wa
kujipikia.
Dkt. Chaula ameyasema hayo mara
baada ya kukitembelea chuo cha afya mazingira-Kagemu kwenye ziara ya
usimamizi shirikishi akishirikiana na TAMISEMI ambao wamefika chuoni
hapo kuona mazingira ya chuo hicho ambacho kilipata madhara ya tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani hapa mwaka 2016.
“Nitaanza ukarabati wa jiko na
darasa,ninamwagiza mkuu wa chuo afanye tahimini ili kila mwanafunzi awe
na utulivu wa mwili na roho”.
Aidha,Dkt. Chaula amekitaka chuo
hicho kuanza mara moja kusafisha eneo la chuo hicho ili waanze
kutengeneza matuta kwa ajili ya kulima bustani ambayo itasaidia
kupunguza gharama ya kununua mahitaji mengine nje ya nchi.
“Uzalendo unaanzia vyuoni hivyo
nitatoa fedha kwa ajili ya vibarua wasafishe eneo la shamba lote na
muanze kulima bustani,lazima mjifunze ujasiliamali mkiwa chuoni”.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Dkt. Hasan Kawia amesema wamepokea maagizo yote na kuahidi
kuyafanyia kazi ikiwemo tatizo la gari la kuwapeleka mafunzo kwa vitendo
wanafunzi hao mipakani
Dkt. Kawia amesema atamfikishia
Katibu Tawala wa mkoa suala hilo kwani serikali bado inawahitaji maofisa
afya katika kulinda jamii isipate magonjwa hususani yale ya milipuko na
vile vile kudhibiti magonjwa kutoka nchi jirani yasiingie nchini.
No comments :
Post a Comment