Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
Standard Chartered, Bw.Sanjay Rughan akizungumza na wadau mbalimbali
katika mkutano wa kutia saini makubalino ya mkopo wa kuwezesha mradi wa
ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR.
Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt.Philip Mpango na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Bw.Sanjay Rughan akitia saini mkataba wa mkopo kwaajili ya kuwezesha
mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.
Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt.Philip Mpango na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Bw.Sanjay Rughan wakionesha mikataba waliosaini kwaajili ya mkopo
utakaosaidia kurahisisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli
Tanzania Mhe.Masanja Kadogoa akifuatilia kikao cha usainishaji wa
mkataba wa mkopo ambao utasaidia kurahisisha ujenzi wa reli ya kisasa wa
SGR.
Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt.Philip Mpango akizungumza na wadau mbalimbali katika mkutano wa
usainishaji wa mkataba wa mkopo wa kuwezesha ujenzi wa mradi wa reli ya
kisasa wa SGR.
Baadhi ya wadau mbalimbali
wakifuatilia mkutano wa usainishwaji wa mkataba wa mkopo wa kusaidia
ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa wa SGR.
Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt.Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered
wakipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali waliowezesha
kufanikisha mkopo wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR.
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO FULLSHANGWE BLOG)
************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali kupitia Wizara ya fedha
imeweza kupata mkopo wa shilingi trilioni 3.3 kupitia waabia 17
wakishirikiana na benki ya Standard Chartered ili
kuwezesha mradi wa
reli ya kisasa kukamilika kwa wakati.
Akizungumza katika hafla ya
usainishaji wa mikataba ya mkopo huo, Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt.Philip Mpango amesema kuwa kila mara wamekuwa wanaomba mabenki ya
hapa nchini kuchangia katika miradi mikubwa ya vipaumbele vya taifa ili
kuweza kufikia malengo yetu kama taifa.
“Mradi huu wa kujenga reli ya
kisasa ni mradi ambao unakwenda kubadilisha maisha ya wananchi
wakitanzania, hivi sasa unavyojengwa unawaajiri watanzania wengi, mradi
huu unatumia baadhi ya vifaa ambavyo vinazalishwa hapa nchini hususani
saruji, mchanga lakini nguvu kazi ni ya vijana wetu”. Amesema
Dkt.Mpango.
Aidha Dkt.Mpango amesema kuwa deni
la nchi yetu bado ni himilivu na ni lazima tukope kwasababu reli hii
tunawekeza takribani miaka 200 ijayo. Hii reli iliyopo (Ya zamani)
imekuwepo takribani miaka 100, hii ya kisasa itakaa zaidi ya miaka 200.
“Kuna baadhi ya waabia wetu tena
wa siku nyingi tuliwaomba waingie kwenye safari hii ya kuchangia mkopo
wala si kama wanatupa bure lakini walinikatalia kwahiyo tunashukuru sana
kupitia kwenu serikali ya Denmark na serikali ya Sweden kuwa waabia
wazuri na marafiki wa watanzania”. Ameongeza Dkt.Mpango.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Standard Chartered, Bw.Sanjay Rughani amesema kuwa zoezi la
kuwekeana saini ya makubaliano ya mkopo kwaajili ya mradi wa reli ya
kisasa ni hatua kubwa hasa katika suala la uchumi pamoja na upande wa
uwekezaji.
“Afrika inabaki kuwa kipaumbele
kwa biashara yetu na wateja kwa ujumla, tunajivunia kutumia utaalamu
wetu kusaidia serikali ya Tanzania na fedha zinazohitajika kwenye mradi
wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR”. Amesema Bw.Sanjay.
Pamoja na hayo Bw.Sanjay amesema
kuwa upatikanaji wa wawekezaji 17 kusaidia mkopo huo ni juhudi kubwa
imefanyika hivyo tutegemee kuwepo kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa
uchumi.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Reli
hapa nchini Mhe.Masanja Kadogosa amesema kuwa mpaka kuwezesha
upatikanaji wa mkopo kwaajili ya mradi huo, kutaongezeka kwa kasi ya
ujenzi huo kwani mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani
Morogoro umefikia asilimia 73, hivyo mkopo huo utawezesha ujenzi wa reli
hiyo kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.
No comments :
Post a Comment