Mkurugenzi wa Idara ya Biashara
Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo
wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja
na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine pichani ni Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za
wateja Vodacom, Celvin Mmasy. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini
Dar Es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Huduma kwa
Wateja Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja
hatuzimi data” ambapo wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa
thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine
pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda
Riwa na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom, Celvin Mmasy.
Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja
Vodacom Tanzania , Celvin Mmasy (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo
wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja
na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine pichani ni Mkurugenzi
wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati)
na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare . Hafla ya
uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo.
…………………………………………………………………………………………………………….
- Menu rahisi, na iliyoko wazi zaidi,
- Bando mpya ya siku 3 za sauti na data ambazo zinatoa thamani zaidi kwa wateja.
Tarehe 13 Februari 2020 Dar es
Salaam. Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza Tanzania
Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza kupunguza bidhaa zake katika
menu
yake kwa asilimia 75 katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja.
Akiongea wakati wa kutoa tangazo
hilo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Bi Harriet
Lwakatare amesema kwamba hatua hii ni mwitikio wa mahitaji ya wateja
ambao walipendekeza kuwa menu iliyopita ilikuwa ni ngumu kuifuata
kutokana na kuwepo kwa chaguzi nyingi.
“Tunakusudia kutoa huduma rahisi
na zilizoko wazi kwa wateja wetu na menu hii iliyorahishwa inahakikisha
kwamba wateja wetu wanaweza kwenda haraka na kwa hatua chache kufikia
huduma wanayoihiji” alisema.
Wateja wa Vodacom wanapata huduma
na bidhaa za kampuni kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo USSD code
ya*149*01#, app ya Vodacom na tovuti ambazo sasa vinatoa chaguzi bora
zaidi.
Kwa upande wake, Bi Linda Riwa,
Mkurugenzi wa Idara ya Bishara wa kampuni ya Vodacom amesema “Sisi pia
tumesikia kile ambacho wateja wetu wanahitaji.
Nina furaha kubwa kutangaza
kampeni yetu mpya ya ‘Wajanja hatuzimi data” inayowapa wateja wetu
unafuu katika matumizi ya intaneti pamoja na uzinduzi wa bando mpya ya
Jimwage ambapo wateja wanaweza kupata GB 3 kwa siku 3 kwa shilingi 2,500
tu. Hii inawezesha kila mtu kutumia mtandao wetu Supa kwa bei nafuu na
kufaidika zaidi.
“Pia tumeboresha huduma yetu ya
sauti ili kuwezesha wateja wetu kuongea na wapendw wao bila kujali
mtandao gani unayoipigia au gharama za ziada kwa mfano huduma yetu ya
cheka iliyoboreshwa inatoa dakika 25 kwa shilingi 500 kupigia mitandao
yote”
Akizungumza kuhusu bidhaa za Data,
Mkuu wa Idara ya bidhaa za wateja Celvin Mmasy alisema, “uzinduzi wa
bidhaa mpya za data zinawezesh kila Mtanzania kuungnishwa kupitia
mtandao Supa wa Vodacom yenye uhakika, sidi kubwa kwa bei hafuu”.
Mwisho
Kuhusu Vodacom:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa
huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa
data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa zaidi ya
wateja milioni 14. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake
tanzu ni sehemu ya Kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group)
iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na
kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom
imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN:
TZ1886102715 Stock name: VODA.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu ya: www.vodacom.co.tz
No comments :
Post a Comment