
********************************
Na Mwandishi Wetu, Mara
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samuel
Kiboye (Namba Tatu) amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa
Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuachachuki binafsi dhidi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli.
Amesema barua Zitto aliyoiandikia bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia hivi karibuni kwa ajili ya kuicheleweshea Serikali mkopo wa zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuboresha elimu, ni jambo mbalo linaonyesha chuki binafsi kwa Serikali.
“Sikufikiria kama ndugu Zitto ambaye ni msomi mwenye uelewa mpana wa mambo angeandika barua ile, ndiyo maana ni vema kabla ya kufanya uamuzi wa namna yoyote lazima ujipe tafakari ya kutosha kwanza.
“Hatua ile inanyesha ni kwa namna gani ndugu Zitto anataka sifa za bure kwa nchi za Ulaya, ila atambue kuwa hakuna Mzungu ambaye ana urafiki wa kudumu na mtu, wao uyapa kipaumbele maslahi yao kwanza, hivyo hali ile ilidhirisha ni kwa namna gani ana chuki binafsi dhidi ya Serikali ya Awamu Tano, lakini atambue kuwa hakuna wa kuikwamisha Serikali yetu, sisi wananchi tumeamua iwe jua au mvua kushirikiana nayo ili kuharakisha maendeleo,”alifafanua Kiboye.
Aidha, alisema kitendo hicho cha
Zitto ni sawa na kuhujumu juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo ni
inashangaza kuona Mtanzania anafanya mambo ya ajabu kwa ajili ya
kuhujumu Serikali iliyopo madarakani.
Pia aliainisha kuwa, kuna makundi
mengi ya Watanzania ndani na nje ya nchi ambao wanadhamira mbaya kwa
juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli,
lakini yatambue kuwa kwa maombi ya Watanzania na kufanya kazi kwa bidii
njama zao hazitafanikia.
“Kila jambo analotekeleza Mheshimiwa Rais Magufuli wao
wanaona halina faida, walianza na ndege, baada ya kuona zinakuja kwa
kasi na matengenezo makubwa ya viwanja vya ndege,wakahamishia lawama
miradi ya reli na Mradi wa Ufuaji Umeme katika bwawa la Julius Nyerere,
ambayo unatekelezwa kwa fedha za ndani,wao kazi kushinda mitandaoni muda
wote kuilamu Serikali, niwaambie huo ni utoto, kila mmoja aonyeshe
uzalendo na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali yetu ili
kutuletea maendeleo. Na watabakia kushangaa sana maana kila mradi
utafanikiwa licha ya mapingamizi yao,” alifafanua Kiboye.Wakati huo huo, Kiboye alimpongeza Rais Dkt.Magufuli kwa kuendelea kuwa na moyo wa ujasiri katika kuwatumikia Watanzania, licha ya vikwazo vingi anavyotengenezewa na wenye chuki binafsi.
“Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli
unafanya kazi nzuri na hakika Mungu atazidi kukushindia vikwazo vyovyote
unavyokumbana navyo kutoka kwa wenye chuki binafsi, sisi Watanzania
tuko bega na wewe na Wana Mara wanakupenda sana na wanazidi kukuombea
wewe na wasaidizi wako,”aliongeza.
No comments :
Post a Comment