*************************
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
George Simbachawene amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Mtume na Nabii
Boniface Mwamposa baada ya kutoroka mjini Moshi kufuatia vifo vya watu
20 ambao walikuwa wanakanyaga mafuta ya upako mahala alipokuwa
akihubiri.
Akizungumzia tukio hilo, Waziri
Simbachawene amesema serikali inafikiria kutengeneza kanuni za
uanzishwaji wa huduma za kiroho kuwa lazima mchungaji awe amesomea
theolojia.
Mtume Mwamposa atapelekwa mjini Moshi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
No comments :
Post a Comment