Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera
akimkabidhi mwalimu Renatus Ngairo kiasi cha shilingi milioni 24 za
mafao yake. Wengine ni viongozi mbalimbali wa TAKUKURU mkoa wa Katavi
Mke wa mwalimu Ngairo bi. Joyce Siza akilia kwa furaha baada ya fedha hizo kuokolewa
………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa mkoani Katavi imefanikiwa kurejesha kiasi cha shilingi milioni 29
za mafao ya mwalimu mstaafu Renatus Ngairo mkazi wa Kawajense katika
Manispaa ya Mpanda zilizokuwa zimechukuliwa na mfanyabiashara mmoja kwa
madai kuwa alikuwa akimdai mstaafu huyo
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi; wakati wa kukabidhi kiasi hicho cha fedha; Mkuu wa
TAKUKURU mkoa wa katavi Christopher Nakua amesema mtuhumiwa
alimnyanga’nya mwalimu huo mafao yake yote kiasi cha shilingi milioni
49 mwezi Novemba mwaka jana mara baada ya kuzitoa benki
Mkuu huyo wa TAKUKURU ameendelea
kueleza kuwa mlalamikaji alifika ofisini kwao na kutoa malalamiko ambapo
walianza kazi ya uchunguzi na mtuhumiwa alikiri kuwa alichukua fedha
hizo kwa madai kuwa alikuwa akimkopesha mwalimu kwa muda mrefu na riba
ikaongezeka
“Hata hivyo riba yenyewe haikuwa
na viwango vya kueleweka hivyo mtuhumiwa amerudisha fedha taslimu
shilingi milioni 24; na ameahidi kumalizia milioni tano baada ya mwezi
mmoja” alisema Nakua
Kwa upande wake Mwalimu Ngairo
amesema alikuwa akikopa fedha kidogo kidogo kutoka kwa mfanyabiashara
huyo hadi deni lake likafikia shilingi milioni 16.4;
“Siku ya tukio alinifuata nyumbani na kuniambia mafao yako yametoka twende ukachukue fedha unilipe deni langu” alisema Ngairo
Ameendelea kueleza kuwa mara
baada ya kutoa kiinua mgongo chake cha shilingi milioni 49 mtuhumiwa
alimnyang’anya begi zima na kumpa milioni tatu tu
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Juma Homera ametaka wafanyabiashara wanaokopesha kwa riba
kufuata taratibu za kifedha zilizowekwa
“Hawa wamezidi sasa hapa mkoani
wamekuwa wakipora fedha za watu kwa madai ya riba kuongezeka, serikali
hii haitavumilia wanyonge kunyanyaswa” alisema Homera
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Katavi
ameisifu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa kazi nzuri
wanayoifanya ya kutetea wanyonge
No comments :
Post a Comment