Baadhi ya wabunge wakipatiwa
semina kuhusu kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu
sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini
Dodoma
Mbunge wa jimbo la
Busega,Mkoani.Simiyu Mhe. Dkt. Raphael Chegeni,akizungumza kwenye semina
kuhusu kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya
mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mratibu wa Malaria na udhibiti wa
wadudu wadhurifu Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Bi. Stella Kajange,akizungumza mara baada ya kutoa
semina kwa wabunge kuhusu utumiaji wa kadi ya alama (score card) ili
kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika
bungeni jijini Dodoma
Sehemu ya waandaaji waa semina
kwa wabunge yenye lengo la kuelimisha kuhusu kutumia kadi ya alama
(score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria
iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mwenyekiti wa wabunge wa chama cha
kupambana na malaria (TAPAMA) Bi. Riziki Lulida ambaye pia ni Mbunge wa
Lindi ,akizungumza kwenye semina iliyokuwa inawahamasisha wabunge
kutumia kadi ya alama kupata takwimu sahihi juu ya kutokomeza ugonjwa wa
malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mbunge wa jimbo la
Busega,Mkoani.Simiyu Mhe. Dkt. Raphael Chegeni,akionyesha kadi ya alama
(score card) jinsi ya kutumia ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa
ugonjwa wa malaria.
Mkurungezi wa Mkusanyiko wa Marais
wa Afrika waliyoungana pamoja kutokomeza Malaria (ALMA) Bi. Joyce
Kafanabo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada
ya kumaliza kutoa semina kwa wabunge jinsi ya kutumia kadi ya alama
(score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa
malaria.
Wabunge pamoja na washiriki wa semina ya kutumia kadi ya alama (Score card) wakiwa katika picha ya pamoja bungeni jijini Dodoma
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wabunge wametakiwa kutumia kadi ya
alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa
malaria katika kuandaa bajeti sahihi ili kuweza kutokomeza malaria
nchini.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti
wa wabunge wa chama cha kupambana na malaria (TAPAMA) Bi. Riziki Lulida
ambaye pia ni Mbunge wa Lindi leo jijini Dodoma wakati wa
kikao cha
uhamashaji wabunge kutumia kadi ya alama kupata takwimu sahihi juu ya
kutokomeza ugonjwa wa malaria.
Bi. Lulida amesema kuwa utumiaji
wa kadi ya alama utasaidia wabunge na jamii kwa ujumla kupata takwimu
sahihi juu ya malaria na kujua namna ya kuweza kujikinga na kujua mkoa
gani unafanya vyema katika kutokomeza malaria.
Akizungumza Bi. Lulida amesema
kwasasa mvua nyingi zinanyesha katika maeneo mengi hapa nchini hivyo
kuna haja ya kusambaza vyandarua katika maeneo hayo kwani mvua hizo
zinatengeneza mazalia ya mbu.
“Baadhi ya maeneo nchini yamepata
mafuliko hivyo mamlaka husika wanatakiwa kugawa vyandarua katika maeneo
hayo kwani mazalia ya mbu yatakuwa yameongezeka kutokana na mvua hizo”,
ameeleza Bi. Lulida.
Naye Mkurungezi wa Mkusanyiko wa
Marais wa Afrika waliyoungana pamoja kutokomeza Malaria (ALMA) Bi. Joyce
Kafanabo amesema kuwa mfumo huo wa kutumia kadi ya alama unawasaidia
wataalam wa malaria kuweza kujaza taarfa zao juu ya kutokomeza malaria
na kujua mpango kazi gani ipo katika mfumo huo ili kutokomeza malaria.
“Wabunge ni wadau wakubwa kwani ni
watunga sera na sharia za nchi hivyo wakipata kutumia kadi hii kwa
ufasaha itasaidia katika kutengeneza bajeti zao katika kutekeleza
majukumu yao katika kutokomeza malaria nchini” amesema Bi. Kafanabo.
Pia Bi. Kafanabo amesema kuwa
wabunge wanawakilisha indadi kubwa ya watanzania hivyo watafanya
uhamasijaji katika majimbo ili wapiga kura wao kuleta utekelezaji wa
kutokomeza malaria kwa kutoa ushirikiano wakutosha kwa serikali na
wataalamu kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu Malaria na udhibiti wa wadudu wadhurifu Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Bi. Stella
Kajange ameeleza kuwa kadi ya alama itasaidia serikali kufatilia afua
mbali mbali zinazotekelezwa na kufatilia utekelezaji wa kutokomeza
malaria nchini.
“lengo ni kuhamasisha wabunge
waweze kuielewa Malaria score card,na weweze kuitumia kufuatilia
utekelezaji wa malaria katika mikoa na Halmashauri,pia lengo lingine ni
kuhamasisha wabunge weweze kutetea bungeni bajeti yabutekelezaji wa afua
za malaria iongezwe hasa kutokana na ongezeko la afua /intervention za
malaria zilizoongezeka mfano upuliziaji wa viuadudu ktk mazalia ya mbu
yaliyotambuliwa”amefafanua Bi Kajange.
Aidha Bi.Kajange amesema kuwa
score card itawawezesha viongozi na watendaji katika ngazi ya
kitaifa,Mkoa na Halmashauri kufanya ufuatiliaji wa karibu juu ya
mwenendo wa utekelezaji wa afua(interventions)za malaria,kugundua
changamoto,kuandaa mpango kazi na mikakati kwa ajili ya kutatua tatizo
No comments :
Post a Comment