Tanzania imesema hakuna katazo kwa Mtanzania yeyote aliyeko nje ya Nchi, China ikiwemo anayezuiwa kurudi Tanzania pindi atakapo.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji
Mnyepe amewaondoa wasiwasi Watanzania hasa wale wanaotaka kusafiri
kwenda ama kurudi kutoka China,na kwamba wale wanaotaka kusafiri kwenda
China tayari waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ameshatoa
maelekezo lakini kwa wale wanaotaka kurudi kutoka China Ubalozi wa
Tanzania Nchini China unashirikiana nao kuwarejesha Tanzania kwa wale
wanaotaka na kwamba hakuna katazo la kurejea Tanzania.
No comments :
Post a Comment