………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Watanzania wametakiwa
kupenda na kutangaza vitu mbali mbali ambavyo vinazalishwa hapa nchini
kwa lengo la kusaidia kuonyesha Uzalendo kwa Taifa.
Akizungumza kwenye
uzinduzi wa Ofisi ya shirika la Ndege la Tanzania ATCL Mkuu wa mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo kwenye hafla iliofanyika kwenye Jengo la Mafao house
jijini Arusha alisema kuwa Uzalendo ni jambo jema na linahitaji Sana
kwa watanzania kuitangaza shirika hilo na kuliunga mkono.
Alisema kujivunia
uwepo wa shirika hilo ambalo linaitangaza Tanzania kote linapoenda
sanjari na kuongeza watalii wanaokuja kuitembelea nchi yetu hivyo
kuongeza pato la taifa.
Aliipongeza Bodi ya
wakurugenzi wa shirika la Ndege kwa kazi nzuri ya kuendelea kuliboresha
shirika hilo na kuwaomba watanzania kulipenda na kujivunia shirika hilo.
Awali akimkaribisha
mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa
shirika hilo mhandisi Emmanuel Koroso alisema kuwa shirika limejipanga
kuhakikisha linaenda na hadhi ya shirika la Ndege nchini ndio maana
wakafungua ofisi hizo zinazoendana na hadhi ya shirika hilo.
Alisema shirika hilo
limeamua kuendana na mageuzi makubwa ya kiundeshaji kuendana na
kuhakikisha shirika hilo linaenda na malengo na matarajio ya serikali ya
awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli kuwa shirika Bora lenye
kuchangia kukuza uchumi wa watanzania.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa shirika hilo Ladslaus Matindi alisema ofisi hiyo
itahudumia na kusimamia pia Ofisi za mkoa wa Kilimanjaro ambapo
aliwataka watanzania kutumia usafiri huo kwa sasà wanafika katika mikoa
10 nchini lengo likiwa kufikia mikoa yote.
No comments :
Post a Comment