Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania TMA Dk. Agnes Kijazi akizungumza wakati akitangaza
taarifa ya utabiri wa hali ya MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA KWA
KIPINDI CHA MWEZI MACHI HADI MEI 2020 katikati ni Dk. Hamza Kabelwa
MKurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA na kushoto
ni Rose Senyagwa Mtaalam wa Hali ya Hewa.
Rose Senyagwa Mtaalam wa hali ya
hewa kutoka TMA wakati akitoa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa msimu
uliopita kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi )katikati ni Dk. Hamza Kabelwa
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.
Baadhi ya vielelezo vya utabiri wa mvua hizo za masika.
………………………………………………………
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Hali ya Hewa Nchini TMA Dkt. Agnes Kijazi leo ametangaza taarifa ya
utabiri wa hali ya hewa mwenendo wa mvua za masika katika kipindi cha
Machi – Mei, 2020 wakati alipozungumza na
waandishi wa habari katika
makao makuu ya taasisi hiyo Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Dk. Kijazi ametoa taarifa
inayotoa uchambuzi wa mwenendo wa mvua za masika katika kipindi cha
Machi – Mei, 2020 ikiwa ni pamoja na mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo
wa msimu.
Ametoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile Kilimo
na Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa ili kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo.

Taarifa hiyo imeelezea utabiri
huo imesema kuwa mvua za Masika kwa kipindi cha Machi hadi Mei, 2020
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mkoa
wa Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba, maeneo mengi ya mikoa ya Arusha,
Manyara na Kilimanjaro, mashariki mwa mkoa wa Geita pamoja na mikoa ya
Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Maeneo ya mkoa wa Kagera,
magharibi mwa mkoa wa Geita, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma, Dar es
Salaam, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na kaskazini mwa
mkoa wa
Morogoro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Morogoro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Taarifa hiyo imeelezea kwamba
Mvua za nje ya msimu zinazoendelea kunyesha katika maeneo yanayopata
misimu miwili ya mvua kwa mwaka, hususan yaliyopo katika pwani ya
kaskazini zinatarajiwa kuendelea na kuungana na msimu wa mvua wa Masika
2020.
Athari zinazotarajiwa ni pamoja
na Mvua za kutosha katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani
hadi juu ya wastani, zinatarajiwa kunufaisha uzalishaji wa mazao
mbalimbali yakiwemo yale yanayostahimili unyevunyevu mwingi ardhini kama
vile mpunga. Aidha, uwepo wa malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya
mifugo na wanyamapori vinatarajiwa ambapo milipuko ya magonjwa na wadudu
waharibifu vinaweza kujitokeza kutokana na hali ya unyevunyevu na
kutuama kwa maji.
Taarifa hiyo imetahadharisha kuwa
Uchimbaji wa madini ufanyike kwa kuzingatia utabiri uliotolewa kwani
ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha maporomoko ya ardhi
hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya
wastani.
Imeeleza kuwa vipindi vifupi vya
mvua kubwa vinaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata
mvua za wastani hadi chini ya wastani, hivyo jamii inashauriwa kuchukua
hatua stahiki
kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
Taarifa imeongeza kuwa Msimu wa
mvua za Masika ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu
kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya
kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia
Tanga na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na
visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera,
Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa
wa Kigoma.
Kutokana na mifumo ya hali ya
hewa ilivyo kwa sasa na jinsi inavyotarajiwa kuwa kwa kipindi chote cha
msimu (kama ilivyoelezwa katika kipengele cha III cha taarifa hii), kwa
ujumla
mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
Hata hivyo, maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki,
mashariki na kusini mwa Ziwa Viktoria, mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani. Aidha, maeneo ya magharibi mwa Ziwa Viktoria na maeneo mengine ya pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es salaam, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro) yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

Taarifa hiyo ya hali ya hewa
inaendelea kueleza kuwa Kanda ya Ziwa Viktoria: (Mikoa ya Kagera, Geita,
Mwanza, Shinyanga, Simiyu, na Mara): Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani
hadi juu ya wastani katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Geita, mikoa
ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara. Aidha, mvua za wastani hadi
chini ya wastani zinatarajiwa katika mikoa ya Kagera, magharibi mwa mkoa wa Geita na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (Wilaya za Kakonko na Kibondo). Mvua hizi zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Machi, 2020 na kuisha kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Mei, 2020.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini:
(mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro
pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani
hadi juu ya wastani katika maeneo ya mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba. Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha
Mafia) pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro yanatarajiwa
kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani. Mvua katika maeneo haya
zinatarajiwa kuanza kati
ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi 2020 na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu ya mwezi Mei, 2020. Aidha, mvua zinazoendelea katika maeneo haya zinatarajiwa kuungana
na mvua za msimu wa Masika, 2020.

Taarifa hiyo imemalizia kuwa
Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Arusha, Manyara na
Kilimanjaro): Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani
katika maeneo mengi.
Mvua hizo zinatarajiwa kuanza
kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi, 2020 na kuisha kati ya
wiki ya pili na tatu ya mwezi Mei, 2020.
No comments :
Post a Comment