Muonekano wa vitanda na vifaa vya
matibabu ndani ya Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na
Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo
Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt.
Binilith Mahenge akiwa na Naibu balozi kutoka Israel Mhe. Eyal David
wakifungua kitambaa, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Kitengo cha
matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika
Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt.
Binilith Mahenge akiongoza zoezi la kukata utepe, ikiwa ni ishara ya
uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi
kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Muonekana wa Jengo la Kitengo cha
matibabu ya magonjwa ya dharura na majeruhi kanda ya kati katika
Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt.
Binilith Mahenge, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya
Dkt. Leonard Subi baada ya tukio uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya
Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya
Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
…………………………………………..
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-DOM
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt.
Binilith Mahenge, leo amezindua Kitengo cha
matibabu ya Magonjwa ya
Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa
Jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo Mhe. Dkt.
Binilith Mahenge amesema kuwa, kitengo hiki ni mkombozi kwa wanachi wa
Kanda ya kati hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma
umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza
matukio ya ajali na magonjwa ya dharura.
“Kitengo hiki ni mkombozi kwa
Wanachi wa Kanda hii hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma
umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza
matukio ya ajali na magonjwa ya dharura jijini na maeneo yanayozunguka
jiji la Dodoma,” alisema.
Aliendelea kusema kuwa, Hospitali
ya Benjamin Mkapa pamoja na huduma zingine za afya ilianzishwa ili
kutoa huduma za Kibingwa, hivyo Serikali inategemea kuona kitengo hiki
kikitoa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya dharura na majeruhi.
Aidha, Dkt. Binilith Mahenge
amesema, Serikali iliingia makubaliano na Shirika la misaada la Israel
(MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION) kwa
ajili ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa BMH hususan wagonjwa wa
dharula na majeruhi,
Mbali na hayo amesema kuwa,
Shirika hilo limekubali kutoa msaada wa vifaa vya kutoa huduma za
dharula na kwa majeruhi na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya wa
Hospitali ya Benjamin Mkapa juu ya utoaji wa huduma hizo.
“Serikali iliingia makubaliano na
Shirika la misaada la Israel (MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL
DEVELOPMENT COOPERATION) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya
zinazotolewa hususan wagonjwa wa dharula na majeruhi, kwa kuboresha eneo
la kutolea huduma pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya kutoa huduma za
dharula na kwa majeruhi. Vilevile kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya”
alisema.
Kwa upande mwingine amempongeza
Mkurugenzi wa Hospitali ya benjamini mkapa na Watumishi wake wote kwa
jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhudumia wananchi wa Kanda ya Kati
na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wa Dkt. Alphonce Chandika
amesema kuwa, mpaka sasa kitengo hiki cha dharura na majeruhi
kimeshahudumia zaidi ya wagonjwa 3,000.
“Kwa Kanda ya Kati, Kitengo hiki
kiko hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee. Na mpaka sasa zaidi ya
wagonjwa 3,000 wamepata huduma kutoka katika kitengo hiki,” alisema Dkt.
Chandika.
Aidha, Dkt. Chandika amemuomba
Naibu Balozi kuendelea kutoa msaada wa mafunzo mbalimbali kwa watumishi
wa Benjamin Mkapa ili kuwajengea uwezo zaidi katika kitengo hiki cha
dharula na kwenye maeneo mengine ya kibingwa, katika huduma ambazo
zinatarajiwa kuanzishwa ikiwemo huduma za matibabu ya moyo, matibabu ya
saratani, upandikizaji wa viungo.
Nae Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya
Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi
ameishukuru amemuomba Naibu balozi Mheshimiwa Eyal David pamoja na
madaktari alioambatana nao wasisite kuendelea kuisaidia Hospitali hii
pale watakapohitaji msaada toka kwenu, huku akisisitiza kuwa, huu ni
mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na
Serikali ya Israel.
No comments :
Post a Comment