Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’
ya mkoani Shinyanga imetoa msaada wa katoni 50 za vinywaji kwa
wanafunzi wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliopo katika mafunzo
yao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo leo Ijumaa Februari 21,2020, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo
Food Products Ltd, Esme Salum amesema kampuni hiyo imeungana na
wanafunzi wa Jeshi la akiba kwa kuchangia katika kufanikisha mahafali ya
mafunzo yatakayofanyika Machi 4,2020.
“Jambo tumefurahi kuungana na
wanafunzi wa jeshi la akiba kwa kuchangia katika kufanikisha mahafali
yao ikiwa ni sehemu ya utamaduni wetu tuliojewekea kushirikiana na jamii
inayotuzunguka. Tumetoa katoni 50 za vinywaji baridi kati ya katoni
hizo 20 ni za maji na 30 ni za juisi mchanganyiko”,amesema Salum.
Akipokea katoni hizo za vinywaji
baridi, Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti
Geofrey Kamala ameishukuru Kampuni ya Jambo kwa kuwaunga mkono
kufanikisha sherehe ya jeshi la akiba.
“Tuliwaandikia barua Jambo ya
kuomba msaada watuchangie katika mahafali yetu ya jeshi la akiba.Kwa
kweli tunawashukuru sana Jambo wamejitoa kwa moyo mmoja,wametupatia maji
katoni 20 pamoja na juisi katoni 30.
Tunawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika sherehe yetu ya jeshi la akiba Mungu awabariki sana,kazi yenu iendelee kubarikiwa”,amesema Kamala.
Jumla ya wanafunzi 143 wa Jeshi
la akiba kutoka wilaya ya Shinyanga walioanza mafunzo yao Novemba 4,2019
wanatarajia kumaliza mafunzo yao Machi 4,2020.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utengenezaji na
Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum
akishikana mkono na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya
Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala wakati akimkabidhi katoni 50 za
vinywaji baridi kuchangia mahafali ya wanafunzi wa Jeshi la Akiba
yatakayofanyika Machi 4,2020. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum (wa pili kushoto) akikabidhi vinywaji baridi kwa
viongozi wa kamati ya sherehe mahafali ya Jeshi la akiba wilaya ya
Shinyanga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe Sarah Stephen,wa
kwanza kulia ni Katibu wa sherehe Aderick Godfrey akifuatiwa na Mhasibu
wa sherehe Martha Charles.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum akimwelezea Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya
ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na baadhi ya wanafunzi wa Jeshi la
Akiba namna kiwanda cha Jambo kinavyoendesha shughuli za uzalishaji wa
vinywaji baridi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum akieelezea namna wanavyozalisha vinywaji baridi.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba
wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na baadhi ya wanafunzi wa
Jeshi la Akiba wakiangalia namna uzalishaji wa vinywaji baridi
unavyofanyika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum akiendelea kuwatembeza kiwandani wageni wake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa
Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akiendelea
kueleza namna kiwanda cha Jambo kinavyoendesha shughuli za uzalishaji wa
vinywaji baridi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum akiteta jambo na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba
wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala baada ya kutembelea kiwanda
cha Jambo.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba
wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala akiagana na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food
Products Limited’ Esme Salum.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba
wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na wanafunzi wa Jeshi la
Akiba wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products
Limited’ Esme Salum.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment