************************
Na Woinde Shizza,Arusha
Jumuiya ya wazazi
mkoani Arusha Leo imemkabidhi imemkabidhi Mwenyekiti Wa jumuiya ya
wazazi wa chama cha mapinduzi Taifa ,ambaye pia ni mjumbe Wa kamati kuu
shilingi milioni moja kwa ajili ya kumchukulia fomu ya kugombea nafasi
ya Urais kwa awamu ya pili.
Akiongea wakati
akimkabidhi Mwenyekiti huyo fedha hizo Katibu mwenezi Wa wilaya ya
Arumeru ambaye pia ni mjumbe Wa kamati ya utekelezaji Wa jumuiya ya
wazazi mkoa Wa Arusha Joshua Ongura alisema kuwa kutokana na tamko LA
Mwenyekiti Wa jumuiya hiyo Taifa alilolitoa December 2019 katika
kongamano lililofanyika jijini Dar es salam wameona watoe fedha hizo
Alisema kuwa katika
kongamano hill jumuiya ya wazazi iliahidi kumchukulia fomu ya kugombea
urais kwa awamu ya pili Mwenyekiti Wa chama hicho ambaye pia ni Rais Wa
serikali ya awamu ya tano.
Alisema kwakua mkoa
Wa Arusha unaanzia na alama A wameamua kuwa Wa kwanza kumchangia rais
,pia wameona watoe kwakua raid ameweza kutekeleza vyema ilani ya chama
,na kutatua matatizo ya wananchi
Akiongea Mara baada
ya kuipokea Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa Ambaye pia ni mjumbe
Wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Edmond Mndolwa aliwashukuru
jumuiya hiyo kwa moyo walionyesha Wa kutoa fedha kwa ajili ya
kumchukulia Rais fomu ya kugombea katika kipindi kingine
Alisema aluhaidi
Rais kumchukulia fomu ya kugombea katika kipindi kingine ,ambapo alisema
iwapo mikoa yote itatoa fedha hizo itapatikana shilingi milioni
selasini na moja 31 ambayo katika hizo watachikuwa shilingi milioni moja
ya kumchukulia fomu Rais naingine itakayobaki ndio wataifanyia kampeni
Alizitaka mikoa
mingine kuiga na kuanza kumchangia fedha ya fomu Rais kama vile mkoa Wa
Arusha ulivyofanya na ulivyoanza kutoa fedha hizo mapema.
Picha ikionyesha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Hezron Mbise Kulia
akimkabidhi Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe
wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi Edmund Mndolwa fedha zilizochangwa
na jumuiya hiyo mkoa Wa Arusha kwa ajili ya kumchukulia fomu ya
kugombea nafasi ya urahisi John Magufuli kwa kipindi cha awamu yapili
ambapo jumuiya hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni moja wakati
alivyokuwa akihitimisha ziara yake ya Siku tano ya kukagua miradi
iliotekelezwa chini ya ilani ya chama cha mapinduzi katika wilaya ya
zote tano za mkoa Wa Arusha (picha na Woinde Shizza, Arusha.
No comments :
Post a Comment