Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akizungumza jambo wakati wa kukagua mitambo
inayotumika katika kituo cha mafunzo ya kufua umeme kwa kutumia nguvu
ya maji
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akipongezwa na Balozi wa Norway mara baada
ya kuzindua Kituo cha Mafunzo cha kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Wiliam Ole Nasha pamoja na Balozi wa Norway nchini Elisabeth
Jacobsen wakipata maelezo katika moja la darasa la kituo cha mafunzo ya
kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji.
Balozi wa Norway nchini Elisabeth
Jacobsen akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa kituo cha mafunzi ya
kufua umeme jwa kutumia nguvu ya maji wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya mitambo ya mafunzo
katika kituo cha mafunzo ya kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji
kinachimilikiwa na Chuo cha Ufundi Arusha Mkoani Kilimanjaro
……………….
zaidi ya shilingi bilioni 8.5
zimetumika kukarabati na kujenga majengo mpya ya kituo cha
mafunzo ya
kufua umeme kwa kutumia nguvu za maji cha Kikuletwa kinachomilikiwa na
Chuo cha Ufundi Arusha , ATC.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kituo hicho Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole
Nasha amesema uendelezaji wa kituo hicho ni sehemu ya mpango mkakati wa
Serikali wa uboreshaji utoaji wa Elimu ya Ufundi nchini kwa kutoa
mafunzo kwa vitendo. Amesema mfumo huo utawezesha kupata wahitimu walio
mafundi mahiri waliobobea katika fani ya kufua umeme.
“Elimu itakayopatikana hapa
itawasaidia vijana kuitumia elimu hiyo kujiajira kwani kuna fursa nyingi
kwenye kujiajiri kuliko kusubiri fursa chache zilizopo za kuajiriwa,
nina uhakika vijana wanaotoka hapa watakuwa mahiri katika kufua umeme ”
amesema Ole Nasha
Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa
uanzishaji wa Kituo cha mafunzo cha kufua umeme kwa kutumia nguvu ya
maji hapa Kikuletwa umelenga kuongeza watalaamu; hasa mafundi stadi
(artisans) na mafundi sanifu (technicians) ambao atashiriki katika
ufuaji wa umeme kutoka vyanzo vidogo vidogo vya maji na vikubwa pamoja
kufanya tafiti juu ya nishati jadidifu (Research in renewable energy)
ikiwemo uzalishaji umeme kutokana na nguvu ya maji.
Ole Nasha amesema serikali
inatambua umuhimu wa Elimu ya ufundi kuelekea Tanzania ya viwanda ambapo
inaendelea kufanya uwekezaji mkuwa katika vyuo vya ufundi, uwekezaji
ambao umeongeza udahili na ubora katika Elimu ya ufundi. Kutokana na
uwekezaji unaoendelea idadi ya wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya
ufundi imeongezeka kutoka 30,000 mwaka 2015 hadi 151,969 mwaka 2019 pia
inaendelea na ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi 43 kwa gharama ya
shilingi bilioni 92 katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na ujenzi wa
chuo kipya Jijini Dodoma chenye hadhi sawa na ATC au DIT kwa gharama ya
shilingi bilioni 18.
Aidha, Naibu Waziri ameongeza kuwa
serikali imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa Elimu ya Ufundi Afrika
Mashariki (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya dola
za kimarekani milioni 75 unaolenga kuleta mapinduzi katika Elimu ya
ufundi nchini kwa kuvijengea vyuo uwezo ili viweze kuzalisha wanafunzi
wenye ujuzi stahiki, ujenzi wa miundombinu bora, kuweka vifaa na
kuwajengea uwezo wakufunzi.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho
Dkt.Masudi Senzia amesema kuwa tayari kituo hicho kimeanza kupokea
wanafunzi ambao wanapata mafunzo katika fani mbalimbali za kufua umeme
ambapo vijana wanaouzunguka eneo la Kikuletwa wamejitokeza kwa
wingi kwa ajili ya kupata elimu itayowaezesha kujikwamua kimaisha.
Masudi ameongeza kuwa kupitia
ufadhili wa benki ya dunia kituo kitaendelea kupanuliwa ili kiweze
kuhudumia nchi za Afrika Mashariki kama kituo cha umahiri .
Kwa upande wake Balozi wa Norway
nchini Tanzania Elizabeth Jacobsen amesema kuwa Norway itaendelea
kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kwa kuendelea
kusaidia na kuijengea uwezo Vyuo katika masuala ya nishati jadidifu
itakayosaidia kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda.
Balozi Elizabeth amesema kuwa
kituo hicho kitasaidia katika mafunzo ya jinsi ya kuongeza uzalishaji wa
umeme unaotokana na maji katika maeneo mbalimbali nchini huku ukilenga
kujenga wataalamu waliobobea katika kufua umeme.
Mkuu wa Wilaya ya Hai,Lengai Ole
Sabaya amewataka wananchi kushirikiana na kituo hicho katika kulinda
miundombinu iliyoko ili iweze kuwanufaisha vyema watu wa Hai,Tanzania na
Afrika Mashariki kwa ujumla
No comments :
Post a Comment