Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza
katika maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa posta barani Afrika (PAPU)
yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutanp cha Kimataifa jijini
Arusha (AICC).
Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Barani Afrika(PAPU)
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele akisalimiana
na mmoja wa maofisa wa polisi alipowasili katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Jijini Arusha
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa
posta Barani Afrika
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza
na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa posta Barani Afrika katika
maadhimisho ya miaka 40
Dkt.Maria
Sasabo katibu mkuu wizara ya kazi usafirishaji na mawasiliano akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa posta
barani Afrika (PAPU)
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele mmoja wa
washiriki wa maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa posta barani Afrika
Na Vero Ignatus Arusha.
Madhimisho
ya miaka 40 ya umoja wa posta barani Afrika yameadhimishwa leo jijini
Arusha ambapo umoja huo ulianzishwa na Muasisi wa Taifa la
Tanzania Hayati Mwl.JK.Nyerere pamoja na viongozi wenzake ili waweze
kuwa na
sauti moja katika umoja wa posta duniani tangia kuanzishwa kwake mwaka
1980.
Aidha viongozi hao waliona Afrika walikuwa hawajaungana
na dunia katika mambo mbalimbali hivyo wakaamua kuanzisha umoja wa posta ili
waweze kuwa na sauti ya pamoja ili wasikilizwe
na umoja wa dunia kwa masuala ya posta.
Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele amesema kuwa hadi sasa yapo
mambo mengi yamekwisha kufanyika katika kuhakikisha kwamba posta inafanya kazi na
watanzania kwa karibu zaidi ambapo hadi sasa posta zimekuwa kila wilaya
‘’ Hapo muda kidogpo posta ilikuwa haijafanya
vizuri ila awamu ya tano ya dkt magufuli ambaye alifuatilia mambo yote
yaliyoanzishwa na na mwanzilishi wan chi hii pamoja na mambo mengine ameuufufua
umoja huuna umerudi kwa malengo yaleyale yaliyowekwa na waanzilishi
Kamwele amezishauri wanachama wa mashirika ya posta
barani Afrika PAPU kuanza kujikita katika kutoa huduma za kifedha haswa
kutokana na kuwa na mtandao mkubwa katika nchi hizo
''Afrika ina nchi Zaidi ya 54 katika umoja wa
posta zipo nchi 45 ambazo zimesajiunga na umoja huo ambapo makao makuu ya umoja
huo yapo Nchini Tanzania jijini Arusha''
Amesema kuwa ya jan 18 wataweka jiwe la msingi
kwaajili ya kujenga ofisi ya umoja wa posta Tanzania itakayogharimu jumla ya
shilingi bilioni 33 za kitanzania,fedha ambazo asilimia 40%zimechangiwa na
serikali ya nchiwashirika wa post ana asilimia nyingine 40 zimechangiwa taasisi
yay a TCRA.
Kwa upande wake katibu mkuu wa PAPU Younouss Djibrine amesema kuwa nchi wanachama wanatakiwa kuboresha matumizi ya mtandao katika kuboresha huduma zao .
Hata hivyo alisema kuwa bado kuna matumizi makubwa ya teknolojia ya mawasiliano jambo ambalo linahitajika kuboreshwa zaidi
Kwa upande wake Meneja mkuu wa shirika la posta nchi Mhandisi
Hassan Mwang’ombe amesema kuwa upelekaji wa vifurushi kwa wananchi
amesema wanaimarisha huduma za posta kwa kuziunganisha pamoja
na mtandao TEHAMA (ICT) ili wananchi waweze kupata huduma kwa haraka Zaidi
Amewaasa wananchi kutumia huduma za posta kwasababu
wapo wataalam na vifaa kwaajili ya kufanyia ukaguzi mizigo yote kabla ya
kusafirishwa(scanner)hivyo mwananchi anapopata kwa njia ya huduma ya posta
mzigo unasafiri ukiwa salama unakaguliwa
‘’ Serikali haitaki mabasi yasafirishe vifurushi kwasababu
havikaguliwi na haijulikani wamebeba mizigo ya ania gani,wakati mwingine
wanabeba hata madawa ya kulevya ,mihadharati hata mizigo hatarishi kwa binadamu’’alisema
Amesema hadi sasa posta imehakikisha kuwa kila Kijiji kina
namba na kinatambulika sambamba na anwani za makazi ili kuwatambua watanzania na
kumfikia mteja popote alipo bila shaka kwasababu kama mwananchihupati huduma
kama unavyotaka ni tatizo
Amesema
kuwa kutokana na utandawazi kuingi wao kama posta wameugeuza kuwa fursa
ndiyo maana kwa sasa posta wanajitahidi kujikita zaidi ili
kumfikia mtanzania na kuhakikisha anapata habari za vifurushi vyake
popote walipo
Ameeleeza kuwa huduma nyingi zitakwenda vijijini kuwafuata
wananchi ili wasipate tabu ya kutembea kwenda mbali kwasababu hayo ndiyo
malengo ya maadhimisho ya miaka 40 ambayo yamekubaliwa na nchi zote za umoja
wa Afrika pamoja na wapenda maendeleo wote duniani
Mwang'ombe
amesema kuwa hadi sasa kwenye ofisi za kata zipo ofisi za posta
katika utoaji wa huduma wananchi wanapokea huduma kwa njia ya mtandao
kwasababu watananchi wanatumia huduma za vifurushi,barua, fedha na
uduma zingine
''Japo kuwa yapo maendeleo mbalimbali ya kiteknolojia
lakini bado tunasema kuna umuhimu wa bidhaa kusafiri kutoka eneo moja kwenda
nyingine kwani wananchi waanagiza bidhaa mbalimbali kutoka kona zote za dunia''
Maandhimishio
hayo ambayo yanakwenda sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo
la makao makuu ya umoja wa posta Afrika sanjari na harambee ya
kuchangia ujenzi huo ambao utafanyika kesho jijini Arusha.
Shirika
la posta tanzania lilianza mwaka 1994 ambapo kabla ya hapo ilikuwa
imeunganishwa na shirika la posta na simu umoja wa umoja wa posta
Afrika ulianzishwa mwaka januari 1980
No comments :
Post a Comment