Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.
Anna Mghwira akiongea na Wakazi wa Kilimanjaro wakati wa Uzinduzi wa
kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima
ya Afya Mkoani Kilimanjaro, ambapo aliwataka watanzania kujiunga na
Bima ya Afya kabla ya kuugua.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea na Wakazi
wa Kilimanjaro wakati wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi
kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani Kilimanjaro,
ambapo aliwataka watanzania kutoweka rehani maisha yao katika suala la
afya kwa kukosa Bima ya Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.
Anna Mghwira akitoa kadi za bima ya afya kwa baadhi ya wakazi wa
Kilimanjaro waliojiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya, wakati
wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa
Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani humo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.
Anna Mghwira akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya wakazi wa
Kilimanjaro waliojiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya, wakati
wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa
Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani humo.
Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro
wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi
kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani humo.
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
……………..
Na Mwandishi Wetu-KILIMANJARO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
NHIF leo umezindua kampeni ya kuhamaisha wananchi kujiunga na mpango wa
vifurushi katika Mkoa wa Kilimajaro.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira ambaye alikuwa
mgeni rasmi
aliwataka watanzania kujiunga na NHIF ili kuwa na uhakika wa matibabu
badala ya kusubiri kuumwa ndipo waanze kutafuta kadi ya bima ya afya.
“Wakati wa amani ambao ni
wakati upo mzima unatakiwa uwekeze na NHIF kwa kukata kadi ya Bima ya
Afya na wakati wa vita ambao ni wa maradhi NHIF ni wa uokoaji kwa
kujitibia, jiungeni na NHIF ili tuwe na uhakika wa matibabu”-Amesema RC
Mghwira.
Aidha, RC Mghwira ameupongeza
Uongozi wa NHIF pamoja ma Bodi ya Mfuko huo kwa kuja na mpango huu wa
vifurushi vya Bima ya Afya ambao una lengo la kuwajumuisha watanzania
wengi zaidi.
Akiongea katika uzinduzi huo,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mama Anne Makinda amesema kuwa
Mpango wa vifurushi vya Bima ya Afya hauzuii taratibu nyingine za
Serikali ikiwemo Sera ya Afya inayotambua afya bure kwa watu wasio na
uwezo ikiwemo Wazee.
Pia, Mama Makinda alisema kuwa
Tanzania sasa tunaingia katika makundi ya nchi ya uchumi wa kati hivyo
mwananchi kuwa na Bima ya Afya ni muhimu kwani nchi yoyote inayoendelea
kuwa na Bima ya Afya ni suala la msingi sana
Wakiongea kwa nyakati tofauti
wanajumuiya ya Machinga na waendesha bodaboda wameipongeza Serikali kwa
kuona umuhimu wa kuwajumuisha bodaboda na machinga katika mpango wa
Vifurushi vya Bima ya Afya ili na wao wanufaike na matibabu.
No comments :
Post a Comment