Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya bluu) akiwasili katika
ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini
(SHUWASA) kwa ajili ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya SHUWASA leo Alhamis
Januari 9,2020. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
Mhe. Stephen Masele akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi.
Flaviana Kifizi. Wa kwanza kulia mbele ni Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga, Bw. Albert Msovela. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Profesa
Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA.
Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele na
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Gulam Hafeez Mukadam.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua rasmi Bodi Mpya ya SHUWASA.
Wakurugenzi wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini wakimsikiliza Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa.
Wakuu wa taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa SHUWASA wakimsikiliza Waziri wa Maji Makame Mbarawa.
Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Albert Msovela akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack wakati uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana
Kifizi akitoa taarifa kuhusu kazi zinazofanywa na SHUWASA.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake Deogratius Sulla, akitoa taarifa kuhusu bodi iliyomaliza muda wake.
Wadau wa maji wakiwa eneo la tukio.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Wadau wa maji kutoka taasisi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya SHUWASA.
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Bodi
ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Deogratius Sulla wakati wa uzinduzi
wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga
Mjini (SHUWASA).
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi zawadi kwa Aliyekuwa Katibu
wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake, Eng’. Silvester Mahole wakati
wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Shinyanga Mjini (SHUWASA).
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti
wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya
ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA).
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa akikabidhi vitendea kazi kwa Katibu wa
Bodi ya SHUWASA,Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Flaviana Kifizi wakati
wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Shinyanga Mjini (SHUWASA).
Wajumbe wa Bodi Mpya ya SHUWASA wakiwa na vitendea kazi vyao.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akipiga picha ya pamoja na Wajumbe wapya wa bodi ya SHUWASA.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa amezindua rasmi Bodi Mpya ya Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) na kuagiza
Mamlaka hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato akitishia kuvunja bodi
hiyo endapo watashindwa kukusanya shilingi milioni 700 kila mwezi.
Prof.
Mbarawa amezindua Bodi mpya ya SHUWASA leo Alhamis Januari 9,2020
katika ofisi za SHUWASA zilizopo Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali wa maji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.
Akizindua
bodi hiyo ya nane tangu SHUWASA ianzishwe mwaka 1998, itayoongozwa na
Bi. Mwamvua Jilumbi, Prof. Mbarawa aliitaka SHUWASA kukusanya mapato na
kupanua mtandao wa maji kwa kujenga miradi yenye ubora ili kuondoa
changamoto ya maji kwa wananchi.
“Kazi
ya kwanza ambayo natoa kwa bodi hii mpya ni kwamba nataka mkusanye
mapato yasiyopungua shilingi milioni 700 kila mwezi,mkishindwa kukusanya
sitakuwa na msalie mtume kuvunja bodi hii”,alisema Prof. Mbarawa.
“Pesa
mtakayokusanya muitumie kulipa KASHWASA na kupanua mtandao wa maji siyo
kila siku mje kuomba fedha Wizarani. Fedha mnayopata ipelekeni kwenye
miradi na mjenge miradi hiyo nyinyi wenyewe kwa kutumia wakandarasi wa
ndani”,aliongeza Prof. Mbarawa.
Waziri
huyo wa Maji aliitahadharisha bodi mpya ya SHUWASA kutothubutu kutumia
fedha za mapato kujilipa posho na kupeana safari zisizo na tija akisema
SHUWASA siyo mahala pa kula fedha bali ni kwa ajili ya kusaidia wananchi
wapate maji safi, salama na ya kutosha.
“Naagiza
bodi hii iwe inafanya maamuzi kwa wakati,msukume maamuzi yenu yafanyike
kwa haraka kwani Watanzania wamechoka wanataka maji”,aliongeza.
Katika
hatua nyingine alisema changamoto ya Taasisi za serikali ikiwemo Jeshi
la Wananchi (JWTZ), polisi na Magereza kudaiwa na SHUWASA wanaifanyia
kazi na serikali itawalipa huku akishauri taasisi hizo kufungiwa mita za
malipa ya kabla ‘ Prepaid Meter’.
Akitoa
taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA iliyomaliza muda wake ambayo
ilizinduliwa Novemba 14,2016,Deogratius Sulla,alisema taasisi za
serikali hasa idara ya ulinzi na usalama zinasuasua katika kulipa ankara
zake za maji kila mwezi,jambo ambalo linasababisha deni la maji kukua
na kufikia shilingi milioni 949, akieleza kuwa jitihada za kufuatilia
madeni hayo hazijazaa matunda makubwa hivyo kumuomba Waziri awasaidie
kutatua changamoto hiyo.
“Mpaka
mwezi Desemba 2019, JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi 520,244,975.50/=,
Magereza shilingi 256,520,120.50/= na polisi shilingi 172,346,465/=”,alieleza .
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi, alisema hivi sasa mamlaka
imeongezewa maeneo mengine matatu ya kutoa huduma ambayo awali yalikuwa
yanahudumiwa na RUWASA ambayo ni Tinde,Didia na Iselamagazi.
Alisema
SHUWASA hukusanya mapato ya wastani wa shilingi 497,891,531 kwa mwezi
ambacho asilimia tano tu hutumika katika kuongeza mtandao katika maeneo
ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji safi.
Kifizi
alieleza kuwa SHUWASA inahuhudumia wakazi wa Manispaa ya Shinyanga
wapatao 186,671 ambapo hadi sasa jumla ya wakazi 149,710 sawa na
asilimia 80.2 wamefikiwa na huduma ya maji safi.
“Hadi
kufikia Desemba 2019 Mamlaka ilikuwa na wateja wapatao 21,505 na
mtandao wa maji safi wenye jumla ya kilomita 549.12. Mahitaji ya maji
safi kwa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga yanakadiriwa kuwa mita za ujazo
21,266 kwa siku”,alieleza Kifizi.
“Wastani
wa matumizi ya maji kwa siku ni mita za ujazo 12,500 kwa siku sawa na
asilimia 58.8 tu ya maji kwa manispaa yote.Kwa mwezi Desemba 2019
mamlaka ilisambaza maji yenye mita za ujazo 324,357 sawa na wastani wa
mita za ujazo 11,709 kwa siku”,alisema Kifizi.
Aliongeza
kuwa SHUWASA inasimamia na kujenga miradi kwa kutumia wataalamu wa
ndani ‘Force account’ katika wilaya za Shinyanga (Negezi – Mwawaza) na
Kahama (Ngogwa – Kitwana) ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa
matenki na mtandao wa maji safi.
No comments :
Post a Comment