RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akitembelea Ujenzhi wa
Nyumba mpya za Mji wa Kwahani Wilaya ya Magharibi Unguja ikiwa ni
shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika
katika viwanja vya Mradi huo Kwahani Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Waziri
wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa na
(kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Zanzibar.Ndg.Khamis Mussa, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka
56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa
Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, akitowa
maelezo ya Ujenzi wa Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, wakati wa
hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi huo unaofanyika katika eneo
la kwahani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri
Elekezi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Mji Mpya Kwahani Jijini
Zanzibar,kutoka Kampuni ya Arqes Africa Ltd .Rose Nestory na (kulia kwa
Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia
Abdiwawa, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
BAADHI ya Wageni waalikwa na
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, wakifuatilia hafla
ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za Mji Mpya wa Kwahani
Jijini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
BAADHI ya Viongozi wa Idara za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.
Ali Mohamed Shein, akihutubia (hayupo pichani) wakati wa hafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa nyumba za mji mpya wa kwahani jijini
Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
BAADHI ya Masheha wa Shehia za
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakifuatilia hafla ya uwekaji wa jiwe la
nsingi la ujenzi wa nyumba za mji mpya wa kwahani Jijini Zanzibar, ikiwa
ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Zanzibar.Ndg. Khamis Mussa akitowa maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi
wa Nyumba za Mji Mpya wa Kwahani Jijini Zanzibar, wakati wa hafla ya
uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka
56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WAZIRI wa Fedha na Mipango
Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa akizungumza wakati wa
uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za Mji Mpya wa Kwahani
Jijini Zanzibar.ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
BAADHI ya Wananchi wa Kwahani
wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia (hayupo pichani) wakati wa hafla
ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wac nyumba za mji mpya wa kwahani
jijini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa hafla
ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Mji Mpya
wa Kwahani Jijini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika eneo hilo la
ujenzi kwahani ikiwa ni shamrashamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wananchi wa
Kwahani, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi
la ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Mji Mpya Kwahani Jijini
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
……………….
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kabla ya Mapinduzi ya
1964, Wazalendo wa Zanzibar walibaguliwa kwa makaazi kutokana na
uwezo
duni walionao.
Dk. Shein amesema hayo katika
hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Mji mpya wa Zanzibar
eneo la Kwahani, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema wengi wa wananchi
ikiwemo wafanyakazi waliishi katika maeneo ya ng’ambo kwenye makazi ya
nyumba duni, huku wale wenye uwezo wakiishi katika maeneo ya mji Mkongwe
na maeneo mengine ya kati ya mji.
Alisema katika uchaguzi wa
mwisho wa mwaka 1963, Chama cha ASP kupitia Ilani yake ya uchaguzi
kilitowa ahadi ya kuwapatia makazi bora wananchi wote, hatua
iliyofuatiwa na ujenzi wa nyumba za Kikwajuni (nyumba za miguu) mara
baada ya Mapinduzi kupitia msaada wa Serikali ya Watu wa Ujerumani.
Alieleza kuwa Serikali ya
Mapinduzi chini ya Uongozi wa Marehemu Abeid Aman Karume, iliendeleza
dhamira ya kujenga nyumba bora za kisasa hatua kwa hatua, kwa kujenga
nyumba katika eneo la Kilimani na hatimae Michenzani.
Aidha, alisema Mapinduzi ya
1964 yameondowa tofauti ya makazi iliyokuwepo kati ya mji mkongwe na
ng’ambo, ambapo hivi sasa mji wote unaonekana kuwa mmoja.
Alisema Serikali ina mipango
madhubuti ya kuendeleza ujenzi wa nyumba za aina hiyo katika maeneo
mbali mbali ya mji ili kuunganisha mazingira yafanane na majengo ya
Michenzani.
Alisema ujenzi huo
utaunganisha majengo ya Michenzani Maul, eneo la packing pamoja na
nyumba za Michenzani, hivyo kuleta mandhani nzuri ya mji wa Zanzibar.
Aliwahakikishia wananchi
walioondoshwa kupisha ujenzi katika eneo hilo kuwa mara baada ya ujenzi
kukamilika watarudi eneo hilo na kuendelea kuwa wananchi wa Kwahani.
Alisema dhamira ya Serikali ni kuijenga Kwahani mpya ili wananchi waweze kuishi katika makazi bora zaidi na kujiletea maendeleo.
Aidha, alisema mara baada ya
Mapinduzi ya 1964, kuna nyumba kadhaa zilitaifishwa na kuwa mali ya
Serikali, na kubainisha kuwa Serikali kupitia uratibu wa shirika la
nyumba inazifahamu nyumba zote hizo, hivyo akawataka watu kuondokana na
ghilba ya kuhodhi nyumba hizo.
Alisema ujenzi huo pamoja na
mambo kadhaa ya maendeleo yanayoendelea kufanyika hapa nchini ni
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015-2020.
Akigusia suala la malipo ya
fidia kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ikiwemo maeneo ya ujenzi, Dk.
Shein alisisitiza kwa kusema kuwa ardhi na mali ya Serikali, hivyo
akabainisha umakini wa Serikali katika kuhakikisha wananchi wote wenye
haki ya kulipwa fidia wanalipwa kutokana na mali zao na sio umiliki wa
ardhi.
“Serikali inatowa haki ya kutumia ardhi lakini sio yako, ikitaka ina haki ya kumpa mtu mwengine………..”, alisema.
Nae, Waziri wa Fedha na Mipango
Balozi Mohamed Ramia alisema uendelezaji wa makazi bora kwa wananchi wa
Zanzibar, ulitokana na ahadi iliyotolewa katika Ilani ya ASP ya mwaka
1963 ya kuhakikisha wananchi wote wanaishi katika makazi bora.
Alisema hatua ya serikali ya
awamu ya saba iliyo chini ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein ya
kujenga nyumba hizo ni utekelezaji wa mipango iliyoanzishwa na viongozi
waliotangulia, akitoa mfano wa ujenzi wa nyumba za maendeleo katika
maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Alisema ujenzi wa mji mpya wa
Zanzibar eneo la Kwahani unaashiria dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya kujenga miji ya kisasa katika maeneo mbali mbali Unguja na
Pemba.
Aidha, alisema Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 inafikia kikomo mwaka huu,
akabainisha matumaini yake ya kuwepo maendeeo endelevu katika miaka
ijayo kwa kuzingatia urithi wa CCM kutoka vyama vya ASP na TANU.
Balozi Ramia aliushukuru
Uongozi wa Shehiya ya Kwahani, CCM Mkoa Mjini Magharibi pamoja na Kamati
ya Fedha ya Baraza la Wawakilishi kwa kufanya juhudi kubwa kuwahamasiha
wananchi wa eneo hilo kukubali wazo la Serikali la kuanzisha ujenzi
huo.
Mapema, Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Khamis Mussa, alisema ujenzi wa mji mpya wa Zanzibar
eneo la Kwahani unatekelezwa kupitia Kampuni ya Estim Construction Ltd
kwa gharama ya shilingi Bilioni 19.6, ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi
huo ulioanza Oktoba 2, 2019 unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 31,
2020.
Alisema ujenzi huo
utakaohusisha‘Blocks’ tatu utakuwa na nyumba 70 za kuishi na maeneo 56
ya biashara, wakati ambapo Blocks mbili zinazofanana kila moja itakuwa
na majengo mawili pacha yenye nyumba 14 kila moja pamoja na maeneo ya
biashara na kufanya jumla ya nyumba 28 za kuishi .
Alisema ‘Block’ la tatu
litakuwa na jengo moja lenye nyumba 14, ambapo kila nyumba itakuwa na
vyumba vitatu vya kuishi, jiko, choo, stoo pamoja na ukumbi.
Aidha, alisema kila jengo
litakuwa la ghorofa sita, sambamba na mji huo kuwa na barabara za ndani,
matangi mawili ya maji pamoja na huduma za umeme.
Mussa alisema kuwa mradi huo
umezingatia utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini MKUZA 111 pamoja na Ilani ya CCM ya 2015-2020.
Alisema kufuatia ujenzi huo
nyumba 52 zilizokuwa wakiishi wananchi zilivunjwa huku nyingine 10
zikiwa katika hatua ya kuvunjwa ili kutoa nafasi zaidi ya kuendeleza
ujenzi huo, wakati ambapo Serikali tayari imeshalipa fedha kuwawezesha
wamiliki kukodi sehemu nyingine na kufidia usumbufu wa kuhama.
Alieleza kuwa baada ya hatua za ujenzi kukamilika wananchi hao watarudi eneo hilo na kupatiwa nyumba mpya bila malipo ya ziada.
Aliushukuru Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kukubali kuikopesha Serikali shilingi
Bilioni 20 ili ziweze kutumika kuambatana na mahitaji ya mradi
yatavyojitokeza.
Aidha, aliwashukuru wananchi
wa Kwahani kwa uzalendo na kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali
kufanikisha ujenzi wa makaazi mapya.
No comments :
Post a Comment