Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akizungumza na akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa
TRA, Ben Usaje Asubisye, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es
Salaam Januari 9, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka
hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu
zilifanyika awali.
Mnada huo ambao
unahusisha mahindi tani 5,000 na ngano tani 460.12 unafanyika baada ya
wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha, hivyo Serikali
imeamua kuuza ili kufidia gharama zake. Nafaka hizo ziliingia nchini
Machi 2017.
Waziri Mkuu
amesitisha mnada huo leo (Alhamisi, Januari 9, 2020) wakati akizungumza
na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Bw. Ben Asubisye,
ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu
ameagiza kutangazwa upya kwa mnada mwingine wa kuuza mahindi hayo
sambamba na ngano na wahakikishe masuala yote kuhusu mnada huo
yanakamilika ndani ya siku tatu kuanzia leo tarehe 09 Januari 2020.
“Mahindi yameuzwa
kwa bei ya sh. 340 kwa kilo moja ambayo ni chini na bei ya soko kwa
sababu bei ya mahindi sokoni kwa sasa ni sh. 800. Zabuni imetangazwa kwa
muda mfupi watu wameshindwa kushiriki. Ilifunguliwa saa 8 mchana na
imefungwa saa 5 usiku.”
Kadhalika, Waziri
Mkuu ameutaka uongozi wa TRA uhakikishe mnada unaofuata unakuwa wa
wazi, huru pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa wananchi wote kushiriki
ili kuondoa malalamiko.
“Kwa kuwa mnada
unafanyika kwa njia ya mtandao, hakikisheni matumizi ya mtandao yanakuwa
rafiki kwa wananchi wote watakaovutiwa kuwasilisha zabuni zao.”
Hata hivyo,
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa TRA ishirikiane na mamlaka nyingine za
Serikali kuhakikisha wanunuzi wa nafaka hizo hawaziingizi sokoni kwa
ajili ya matumizi ya binadamu. Nafaka hizo zimepimwa na kuthibitika kuwa
zinafaa kwa matumizi ya wanyama.
No comments :
Post a Comment